|
|
|
KUPANDA MBINGUNI |
|
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “ Basi yule ambaye
Mwenyezi Mungu Anataka kumuongoza, Hufungulia kifua
chake Uislamu; na yule ambaye Mwenyezi Mungu Anataka
kumhukumu kupotea, Hufanya kifua chake kizito kinaona
tabu kubwa (kufuata huo Uislamu); kama kwamba anapanda
mbinguni (kusikokuwa na pumzi). Namna hivi Mwenyezi
Mungu Anajaalia uchafu juu ya wale wasioamini.
Aya ya 125 Suratul
An-am. |
|
UKWELI WA KISAYANSI:
Ujuzi juu ya mpangilio wa anga ulikuwa haupo hadi Pascal
alipothibitisha mwaka 1648 kuwa shinikizo la hewa
hupungua kila unapokwenda juu ya usawa wa bahari.
Ikabainika baadae kuwa hewa iko kwa wingi zaidi katika
tabaka za chini ya angahewa, hukusanyika asilimia
hamsini (50%) ya gesi za anga baina ya usawa wa ardhi
na urefu wa futi elfu ishirini (20,000) juu ya usawa wa
bahari, na asilimia tisini (90%) baina ya usawa wa ardhi
na urefu wa futi elfu hamsini (50,000) kwenye usawa wa
ardhi. Kwa hiyo wingi wake hupungua kila unapopanda juu
kwa ujumla. Na hewa hugotagota kwa kiasi kikubwa katika
tabaka za juu kabla ya kupotea kabisa katika anga. Na
kuwepo kwa binadamu katika muinuko usiopindukia futi
elfu kumi (10,000) juu ya usawa wa bahari,
hakumsababishii tatizo lolote. Chombo cha kuvutia pumzi
kinaweza kuzoea kwenye urefu kati ya futi elfu kumi na
ishirini na tano (10,000 – 25,000). Binadamu kila
anapopaa juu mbinguni, basi hupungua shinikizo la anga
na hupungua kiasi cha oksijeni, jambo ambalo husababisha
kubanwa kwa kifua na tabu kubwa ya kuvuta pumzi huzidi
kutokana na haja kubwa ya tishu (mkusanyiko wa seli
mwilini) ya oksijeni. Iwapo isipokuwepo na seli za mwili
kuzidi kuhitaji ili zifanye kazi zake wakati inapozidi
kupanda juu, hupatwa na hali mbaya mno ambapo uvutaji
pumzi huchafuka (Oxygen Starvation). Kwa
sababu ya upungufu mkubwa wa oksijeni, binadamu wakati
huo hupatwa na kufeli kwa chombo cha kuvutia pumzi (Respiratory
System) na huangamia. |
|
UPANDE WA MIUJIZA:
Ni wazi kuwa binadamu wakati wa wahyi, hakujua suala la
mpangilio wa gesi ya angahewa katika tabaka zake
tofauti, na kwa hiyo hali ya kupungua kwa shinikizo
katika tabaka za juu na kupungua kiasi wingi wa gesi ya
oksijeni ya lazima kwa uhai kila binaadamu anapozidi
kupanda angani, na kwa hiyo hajui athari za hayo kwa
uvutaji wa pumzi na kubakia uhai, kwani humalizikia
kufeli kwa chombo cha kuvutia pumzi. Bali kinyume cha
hivyo, watu walikuwa wakidhani kuwa kila binadamu
anapozidi kwenda juu kifua chake hutanuka zaidi na
kuzidi kufurahia hewa safi.
Aya tukufu inaashiria kwa uwazi kabisa mambo
mawili yaliyogunduliwa na sayansi mpya. Kwanza ni
kubanwa kwa kifua na uzito wa kuvuta pumzi kila binadamu
anapozidi kupanda juu katika tabaka za anga.
Iliyobainika ni kuwa hutokea kwa sababu ya kupungua kwa
oksijeni na kushuka kwa shinikizo la hewa angani. Pili
ni hali mbaya inayotangulia mauti, ni kubanwa kwa pumzi
wakati anapojaribu kupanda tabaka za anga futi elfu
thelathini, kwa sababu ya kushuka sana kwa shinikizo la
anga na upungufu mkubwa wa oksijeni ya lazima kwa uhai
hadi kumalizika kwa oksijeni ndani ya mapafu na binadamu
kufikwa na mauti na kuangamia.
Mbali na neno (anapanda mbinguni) ambapo
kwa maana yake ya Kiarabu inaongeza uzito wakati wa
kupanda. Na huu ni wasfu wa kina wa mashaka na machungu
yanayoambatana na tukio. Hivyo inawezekana habari za
ukweli huu kuwa chengine isipokuwa ni wahyi toka kwa
Mwingi wa kujua na Mwingi wa habari. |
|
|
|
Tafsili:
Kiarabu
 |
|
Kiingereza
Kifaransa Kijerumani Kispani Kituruki
Kiurdu
Kifarsi Kihausa |
|
|