|
|
|
KUINGILIANA NA KUPAMBANUKA KWA
MIKUSANYIKO YA BAHARI |
|
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema,
“ Anazikutanisha bahari mbili (ya maji ya chumvi na ya
maji matamu). Baina yao kuna kizuwizi, haziingiliani
(zikaharibiana kabisa kabisa). Basi ipi katika neema za
Mola wenu mnayoikanusha (kuwa si neema yake)? Katika
hizo bahari mbili, hutoka lulu na marijani.” |
|
UHAKIKA WA KISAYANSI:
Haikuwa ikijulikana kuwa
bahari ya chumvi ni tofauti katika mpangilio na wala sio
bahari moja iliyochanganyika isipokuwa mwaka 1873 wakati
msafara wa Challenger ulipozunguka katika bahari
kwa miaka mitatu. Na katika mwaka 1942, kwa mara ya
kwanza palidhihiri matokeo ya tafiti ndefu
yaliyopatikana kwa kuanzishwa mamia ya vituo vya
baharini katika bahari. Wakakuta kuwa bahari ya
Atlantic kwa mfano, haifanyiki na bahari moja, bali
inafanyika kwa bahari tofauti. Ni bahari moja
inayotafautiana mikusanyiko ya maji katika viwango vya
joto, ukubwa wa eneo, chumvi, viumbe hai vya majini na
kiasi cha kuyayuka kwa oksijeni. Hii ni katika bahari
moja, mbali na bahari mbili zenye kutofautiana kama
bahari ya Mediterranian na bahari ya Sham (Red Sea),
bahari ya Mediterranian na bahari ya Atlantic, na bahari
ya Sham (Red Sea) na ghuba ya Aden. Pia zinakutana
katika mkondo maalumu. Katika mwaka 1942, kwa mara ya
kwanza, imejulikana kuwa kuna bahari zenye kukutana maji
yake, lakini baadhi yake zinatofautiana na nyengine
katika sifa. Maji ya bahari si yenye kutulia, lakini
daima yapo katika harakati zinazoendelea zinazoyafanya
makundi ya maji kuingiliana baina yao lakini kila maji
huendelea kuhodhi sifa zake katika kiasi cha chumvi,
joto, wingi, kupwa na kujaa. Mawimbi, kasi za maji na
pepo, vyote hivyo ni vitendakazi vyenye kuyafanya maji
ya bahari daima kuwa katika harakati, lakini pamoja na
hayo haichanaganyiki mikusanyiko ya bahari yenye
kutofautiana sifa. Kumekuwa na kizuwizi chenye
kutenganisha baina ya bahari mbili zenye kupakana katika
maji au katika mkondo. |
|
UPANDE WA MIUJIZA:
Aya tukufu zinazungumzia
juu ya bahari mbili za chumvi zilizopakana
zilizoingiliana na kila moja inahifadhi sifa zake, na
baina yake kumekuwa na kizuwizi chenye kuzuwia
zisichanganyike. Kutajwa kwa lulu na marijani katika aya
tukufu, ni dalili ya kuwa ni bahari mbili za chumvi,
kwani madini hizo hazipatikani isipokuwa kwenye bahari
za chumvi, jambo ambalo linamaanisha kuwa mazungumzo
yanahusu maji ya bahari za chumvi ambazo zinaonekana
kuwa ni moja zenye sifa moja, lakini kwa hakika ni
mikusanyiko inayopakana na yenye sifa tofauti.
Bahari za chumvi
zinazopakana kwa macho ya kawaida zinaonekana kama ni
mkusanyiko mmoja wa maji yenye sifa moja, lakini kwa
hakika ni mikusanyiko yenye sifa tofauti katika chumvi,
joto na katika wingi. Hayakufahamika hayo isipokuwa kwa
kutumia teknolojia mpya. Pamoja na hayo, Qurani
imezitaja sifa hizo ikajulisha kutofautiana kila bahari
mbili za chumvi zenye kupakana. Kwani ni zenye
kuingiliana baina yao daima na zinachanganyika, na baina
yao kuna kizuwizi kinachozuwia maji yao yasichanganyike.
Hivyo hii sio dalili ya wazi kuwa Qurani ni maneno ya
Mwenyezi Mungu !. |
|
|
|
Tafsili:
Kiarabu
 |
|
Kiingereza
Kifaransa Kijerumani Kispani Kituruki
Kiurdu
Kifarsi Kihausa |
|
|