|
|
|
MAMWAIKIO YA
MITO |
|
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “ Naye (Mwenyezi
Mungu) ndiye Anayeziunganisha bahari mbili; hii ni tamu,
inayoondosha kiu, na hii ni yenye chumvi kali; na
Akaweka kinga kati yao na kizuizi kizuiacho
(zisiharibiane ila pale kiasi cha kukutana tu). Aya
ya 53 ya Suratul Furqan. |
|
UHAKIKA WA KISAYANSI:
Kitabu cha kwanza kudhihiri kuhusu sayansi ya
bahari katika karne ya kumi na nane, maelezo yake
yalikuwa duni. Kisha sayansi ya bahari ikaanza kuchukua
sehemu yake baina ya sayansi mpya wakati meli ya
Challenger ya Uingereza ilipoanza safari yake ya
kuizunguka dunia kuanzia mwaka 1872 hadi mwaka 1876.
Kisha zikafuatia safari za kisayansi za ugunduzi wa
bahari. Mwishoni mwa karne ya ishirini, yakaanza kuzidi
matumaini ya binadamu ya kuifahamu bahari kwa njia ya
setalaiti na upigaji picha wa mbali. Baada ya uchunguzi
wa maeneo mengi ya makutanio ya mito na bahari, watafiti
wamegundua kuwa eneo la mamwaikio ni mazingira pekee
katika sifa zake za kimaumbile na kibayolojia
kulinganisha na mto na bahari licha ya kuingiliana kwa
maji na mwendo wake baina yao kwa mujibu wa kupwa na
kujaa kwa bahari na kufurika kwa mto na ukame wake. Na
yalikuwa ni kizuizi chenye kutenganisha mazingira ya
mamwaikio na mazingira ya mto na mazingira ya bahari.
Eneo hilo hubakia na sifa zake za pekee licha ya sababu
za mchanganyiko kama vile kupwa na kujaa kwa bahari, na
hali za mafuriko na kupungua, ambazo zinahesabiwa kuwa
ni kati ya sababu zenye nguvu za mchanganyiko. Kwa
kutenganisha mazingira matatu, na kwa kuvihesabu viumbe
hai vinavyoishi katika mazingira hayo, eneo la mamwaikio
linahesabiwa kuwa ni chumba cha viumbe hai vingi
vinavyoishi ndani yake. Kwani viumbe hai hivi haviwezi
kuishi isipokuwa katika eneo la mamwaikio lenye sifa za
pekee. Wakati huo huo ni eneo lililohamwa na viumbe hai
vingi vinavyoishi baharini na mitoni, kwani viumbe hai
hivyo hufa iwapo vitaingia katika mazingira hayo kwa
sababu ya tofauti ya sifa zake. |
|
UPANDE WA MIUJIZA:
Mikusanyiko yote ya maji inaweza kuitwa
bahari. Bahari tamu inayoondosha kiu au tamu mno, ni mto
na bahari yenye chumvi kali au chumvi nyingi ni bahari
au bahari ya chumvi. Na kwa hali hiyo, yamevuliwa maji
ya mamwaikio kwani ni mchanganyiko baina ya chumvi na
utamu, hayana sifa ya maji matamu yenye kuondosha kiu
wala chumvi kali. Kwa wasfu huu, maji yako katika
mafungu matatu: Maji ya mto, maji ya bahari, na baina
yao maji ya eneo la mamwaikio lililoelezewa katika aya
tukufu kuwa ni kinga au kizuizi chenye kuzuia kutamba
kwa sifa ya chumvi ya bahari juu ya mto au utamu wa mto
juu ya bahari. Mazingira ya mamwaikio ni chumba kwa
wenye kuishi ndani yake kati ya viumbe hai, na kizuizi
chenye kuzuia wenye kuishi nje yake katika mto au
bahari. Hii maana yake ni kutofautika kwa mazingira
matatu katika sifa za kimaumbile na katika viumbe hai.
Maendeleo ya kihistoria katika mwendo wa
sayansi ya bahari yanashuhudia kutokuwepo kwa maelezo ya
uhakika kuhusu bahari kabla ya mwaka 1400. Pamoja na hayo, Qurani Tukufu imeeleza kwa hakika
kabisa eneo la mamwaikio ya mito. Imebainisha kuwa ni
mazingira ya pekee katika sifa zake za kimaumbile na za
kibayolojia kulinganisha na mazingira ya mto na
mazingira ya bahari. Imeelezea kuwa licha ya kuingiliana
kwa maji na mwendo wake wa kudumu kuelekea kwenye
bahari, basi sifa hizo hubakia thabiti. Unatokea wapi
ujuzi huo katika Qurani bila ya teknolojia na vyombo vya
kisayansi, ikiwa si kutoka kwa ambaye elimu yake
imekizunguka kila kitu?!
|
|
 |
|
Tafsili:
Kiarabu
 |
|
Kiingereza
Kifaransa Kijerumani Kispani Kituruki
Kiurdu
Kifarsi Kihausa |
|
|