|
UPANDE WA MIUJIZA:
Zamani binadamu alikuwa
akiamini mambo mengi ya kijinga kuhusu bahari na bahari
kubwa. Mabaharia wakati huo hawakuwa na maarifa ya kweli
ya kisayansi kuhusu hali zilizoko katika vina virefu vya
bahari. Maelezo kuhusu pepo za bahari yalikuwa haba.
Na haya ndiyo yaliyozuia
mambo ya kijinga kuijua bahari iliyotuama isiyoweza
kupitiwa na meli. Warumi wa kale waliamini kuwepo kwa
samaki wenye kufyonza wenye athari za kichawi katika
kusimamisha mwendo wa meli. Licha ya kuwa watu wa kale
walikuwa wakijua upepo ndio wenye kuathiri mawimbi ya
juu, lakini ilikuwa ni vigumu kujua chochote kuhusu
mwendo wa mawimbi ya ndani katika bahari yenye kina
kirefu. Historia ya sayansi inabainisha kuwa durusu
zisizokatika za sayansi ya bahari na vina vyake,
hazikuanza isipokuwa mwanzoni mwa karne ya ishirini
wakati vilipogunduliwa vyombo vinavyofaa vya durusu
nyeti kama hizo. Sayansi mpya ya bahari, imeweza
kugundua katika nusu ya pili ya karne siri za kushangaza
katika vina vya bahari na bahari kubwa kwa kugundua hali
mbili: Kiza cha bahari yenye kina kirefu, na mwendo wa
mawimbi ya ndani. Aya tukufu imeashiria hali hizi mbili.
Aya tukufu imeashiria
hali ya kiza katika bahari zenye kina kirefu kwa
kuielezea kuwa ni bahari yenye maji mengi, nayo ni
bahari yenye kina kirefu. Na kiza katika bahari hizo ni
kiza chenye kupanda kidogo kidogo. Wanafasiri wamesema:
Makusudio ya viza hivyo ni kiza cha mawingu, kiza cha
mawimbi na kiza cha bahari. Anayekuwa katika viza hivyo,
hawezi kuona chochote. Mawingu mazito yenye kuziba
bahari hizo, huzuia kiasi cha mwangaza wa jua, na
bahari kwa mawimbi yake ya juu, huzuia sehemu nyengine
ya mwangaza huo. Kisha maji hufyonza rangi za jua moja
baada ya nyengine hadi rangi hizo hupotea kabisa. Kisha
inakuja zamu ya mawimbi ya ndani yanayogeuza vina virefu
kuwa ni kiza totoro hata binadamu akitoa mkono wake
hawezi kuuona. Yamekuja maelezo ya kiza juu ya kiza
kuelezea hali katika bahari kwa uwazi kabisa. Pia samaki
katika vina hivyo virefu, hawana macho bali wana viungo
vyenye mwangaza ambavyo Mwenyezi Mungu Ameviumba katika
miili yao kuwaangazia njia yao. Na haya ndiyo maneno
Yake Mwenyezi Mungu, “ Na ambaye Mwenyezi
Mungu hakumjaalia nuru, hawi na nuru.”
Aya pia imeashiria
mwendo wa mawimbi ya ndani katika kauli yake Mwenyezi
Mungu Mtukufu, “ Katika bahari yenye maji mengi,
inayofunikwa na mawimbi juu ya mawimbi.” Maana
yake ni kuwa mawimbi yanafunika bahari yenye maji mengi.
Na haya ndiyo yaliyothibitishwa na wataalamu wa bahari
pale waliposema kuwa bahari yenye maji mengi na yenye
kina kirefu, ni tofauti na bahari ya juu, kwani ndani
yake mna mawimbi katika eneo lenye kutenganisha baina ya
bahari ya juu na bahari yenye kina kirefu, ni tofauti na
mawimbi ya juu, jambo ambalo halikujulikana isipokuwa
tokea miaka mia moja tu.
Ukweli huu wa kisayansi
wa kushangaza umetajwa na Qurani Tukufu tokea karne kumi
na nne. Ni nani aliyemfahamisha Muhammad (S.A.W)? Ni
Mwenyezi Mungu ulio juu utajo Wake.
|