|
|
|
NYOTA
ZINAZOREJEA NYUMA ZINAZOKWENDA NA KUJIFICHA |
|
Mwenyezi Mungu Anasema, “ Basi
Naapa kwa nyota zinazorejea nyuma. Zinazokwenda, kisha
zikajificha.” Aya za 15 na 16 za Suratul At Takwyr. |
|
UKWELI WA KISAYANSI:
Umri wa uzee katika
maisha ya nyota kubwa ni kama tundu nyeusi (Black
holes), kundi kubwa zaidi kuliko jua kwa mara tano
zaidi. Tundu hizo nyeusi zinasifika kwa ukubwa wa eneo
na mvuto mkubwa mno, kwani hakuna kitu kinachokwepa
kabisa hata mwangaza wenyewe ambao kasi yake ni ( kiasi
cha kilometa 300,000 kwa sekunde). Toka hapa basi
limekuja jina lake lenye kuonyesha kuwepo kwa maeneo
kama tundu katika ukurasa wa mbingu uliopotea kila kitu
na kuwa tundu nyingi. Nyota hizi kubwa zenye kupotea au
kuonekana, hufagia kila kitu kinachozikaribia. Kwa hiyo,
yametambulishwa hayo na hesabu zilizoitwa fagio kubwa (Giant
vacuum – Cleaners), nadharia iliyowekwa na
Karl Schwars Child mwaka 1916. Tokea mwaka 1971,
Robert Oppenheimer amezidisha uwezekano wa kuwepo kwake
kwa kuthibisha. Wataalamu wana imani kwamba kundi letu
la nyota kwa mfano ni kama tundu nyeusi. |
|
UPANDE WA MIUJIZA:
Kiapo kimekanusha katika
mtindo wa Qurani Tukufu kwa ajili ya kuthibitisha kama
kwamba Mwenyezi Mungu Anasema kuwa hauna haja ya kiapo
kwa hoja hizo zilizo bayana. Kiapo kimetajwa katika
kuonyesha dalili ya kuwa Qurani Tukufu ni Wahyi wa
Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “
Basi naapa kwa nyota zinazorejea nyuma. Zinazokwenda
kisha zikajificha. Na kwa usiku uingiapo. Na kwa asubuhi
inapopambazuka. Kwa hakika hii (Qurani) ni kauli
(aliyokuja nayo) Mjumbe mtukufu (Jibrili).”
Aya za 15 – 19 za Suratul At Takwyr. Ni zenye kuonyesha
utukufu wa kiapo na umuhimu wake katika kujulisha chenye
kuapiwa. Na hapa kimetajwa kwa sifa ambazo zinakutana
sawasawa na sifa za kinachoitwa tundu nyeusi. Katika
asili yake, ni nyota zinazokwenda katika mizunguko yake.
Kwa hakika ni nyota kubwa ambazo mwisho wa umri wake
zimeporomoka, ikanywea mada yake, zikajificha na
hazidhihirishi mwangaza wowote. Sababu ya hayo, ni
ukubwa wa mvuto wake ambao unazifanya zifagie kila kitu
kilicho pembeni yake katika njia yake na kukimeza kwa
hiyo huzidi ukubwa wake na nguvu yake. Hapa unadhihiri
wasfu wake wa (zinazokwenda kisha zikajificha) au
mafagio makubwa. Ujuzi wa sifa hizo ni mpya kwa hiyo
kutajwa kwake katika Qurani kwa maneno yenye kuzijulisha
kwa kina, ni katika kuthibitisha wahyi wake wa dalili
tosha kuwa ni maneno ya Mwenyezi Mungu Muumba. |
|
 |
|
Tafsili:
Kiarabu
 |
|
Kiingereza
Kifaransa Kijerumani Kispani Kituruki
Kiurdu
Kifarsi Kihausa |
|
|