Bodi ya Kimataifa Ya Miujiza Ya Kisayansi Ya Qurani Na sunna    
Risala yetu: Kudhihirisha miujiza ya kisayansi Na kuihakiki na kuichapisha.

Lugha

Ukurasa Kuu Muhtasari Wa Utafiti Kuhusu Bodi Wasiliana Nasi  

ENEO LA CHINI KABISA JUU YA USO WA ARDHI

Mwenyezi Mungu Amesema,  “ Warumi wameshindwa. Katika nchi iliyo karibu (na nchi ya Bara Arabu. Nayo ni Shamu); nao baada ya kushindwa kwao watashinda. Katika miaka michache; amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla (yake) na baada (yake); na siku hiyo Waislamu watafurahi.”

UHAKIKA WA KISAYANSI:

          Vitabu vya historia vinaelezea kutokea kwa vita baina ya malaka mbili ya Waajemi na utawala wa Bezante, nayo ni sehemu ya mashariki ya utwala wa Warumi, katika eneo la baina ya Azriat na Basry karibu na bahari maiti (Dead Sea) ambapo Waajemi walipata ushindi mkubwa mno kuwashinda Warumi na hiyo ilikuwa katika mwaka 619 AD.

         Warumi wa Bezante wakapata hasara kubwa mno katika vita hivyo na wote walioishi wakati huo wakategemea kuwa wataangamia kabisa na utawala wao. Lakini yalitokea yale ambayo hayakutegemewa. Katika mwezi wa Desemba mwaka 627AD, vilitokea vita vya mwisho baina ya Wabezante na utawala wa Waajemi katika eneo la Nineveh.  Warumi wakawashinda Waajemi. Na baada ya miezi michache, Waajemi walitaka kutia saini mkataba na Wabezante uliowalazimisha kuzirejesha ardhi walizozichukua kwao.

         Picha za kijiografia za maeneo ya mabonde ya ardhi duniani zinaonyesha kuwa eneo lililo chini kabisa  juu ya uso wa ardhi ni lile eneo lililo karibu na bahari maiti (Dead Sea) nchini Palestina, kwani liko chini ya usawa wa bahari kwa kina cha meta 395. Yamethibitishwa hayo na picha na vipimo vya setalaiti.

UPANDE WA MIUJIZA:

          Kuna pande mbili za miujiza katika aya hizi tukufu. Kwanza ni kule Qurani tukufu kuelezea ushindi wa Warumi kuwashinda Waajemi baada ya kushindwa kwao vibaya sana, baada ya miaka kadhaa. Na miaka kadhaa maana yake ni miaka baina ya mitano na saba, au baina ya mwaka mmoja na miaka tisa, kama wasemavyo wataalamu wa lugha. Yametimia yaliyoahidiwa na Qurani tukufu baada ya miaka saba, kwani vilitokea vita vyengine baina ya Waajemi na Warumi mwaka 627AD na Warumi wakashinda. Haya yamekwenda sambamba na ushindi wa Waislamu kwa washirikina wa Qureish katika vita vikubwa vya Badr. Ushindi huo ulionekana mgumu katika macho ya Waarabu washirikina kwa kiasi ambacho wakaanza kuwakejeli kutokana na aya hizi za Qurani na wakaweka rehani kwa Waislamu ikiwa utapatikana ushindi huo unaodaiwa. Yakapotea matumaini yao na ukatimia muujiza wa Qurani Tukufu wakati watu walipotoa mapema habari za ushindi wa Warumi.

         Upande wa pili wa miujiza katika aya hizi tukufu ni kuwa umetokea ukweli wa kijiografia uliokuwa haujulikani na yeyote katika wakati huo. Aya zimeelezea kuwa Warumi watashindwa vita na Waajemi kwenye eneo lililo chini kabisa katika ardhi. Neno (Adna) katika Lugha ya Kiarabu lina maana mbili, karibu na chini zaidi. Kwa upande mmoja ni eneo la karibu zaidi na Bara Arabu, na kwa upande mwengine ni eneo lililo chini kabisa juu ya uso wa ardhi, kwani liko chini ya usawa wa ufukwe wa bahari kwa futi 1312 (kiasi cha meta 400). Nalo ni eneo lililo chini kabisa kurekodiwa na setelaiti juu ya eneo kavu. Pia yameelezwa hayo na kamusi ya Uingereza. Na ukweli wa kihistoria unahakikisha kuwa vita vimetokea katika maeneo ya dunia yaliyo chini zaidi ya bonde la Bahari Maiti (Dead Sea) ambayo yasingeweza kupimwa katika hali ya kutokuwepo kwa teknolojia ya vipimo ya kisasa. Kwa hiyo ilikuwa haiwezekani kwa mtu yeyote wakati huo kujua kuwa eneo hilo ni eneo lililo chini kabisa duniani. Je, hivyo hii sio dalili ya kwamba Qurani  ni wahyi na inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “ Sema: Namshukuru Mwenyezi Mungu, Atakuonyesheni aya zake na mtazijua.”

Tafsili: Kiarabu   

              Kiingereza   Kifaransa     Kijerumani      Kispani      Kituruki       Kiurdu    Kifarsi     Kihausa

Bodi ya Kimataifa Ya Miujiza Ya Kisayansi Ya Qurani Na sunna   (1428-2007)