|
UKWELI WA KISAYANSI:
Kifupa
ndugu
katika elimu ya vijusi ni (
mchirizi wa asili ):
Elimu ya kileo ya
vijusi imeweka wazi kuwa kifupa ndugu, ni mchirizi wa
asili ( Primitive Streak ), kwani mchirizi huu wa
kwanza ni wenye kufanyika mara tu baada ya kudhihiri kwa
kijusi kwa tabaka zake zote na hasa chombo cha mishipa
ya fahamu. Kisha mchirizi huu hutoweka na hakuna
kinachobakia isipokuwa alama ambayo huitwa mfupa wa
kifupa ndugu.
Kufanyika kwa
mchirizi wa asili: Katika siku ya kumi na nne,
kinakuwa pembe nne visahani vya nje na ndani katika seli
za kijusi hadi ziwe katika umbo la pea, na sehemu pana
huwa ni sehemu ya mbele wakati ambapo sehemu ya nyuma
inagonga, na huchangamka seli za kisahani cha nje
( Ectoderm) katika sehemu ya nyuma yenye kufanya
mchirizi wa asili (Primitive Streak ) ambao hudhihiri
kwa mara ya kwanza katika siku ya kumi na tano tokea
kuanza kwa mchevuko.
Hudhihiri mgawanyiko wa
haraka na ukuaji mwingi wa mchirizi wa asili na
huondoka kwenye seli kuliani kwake na kushotoni kwake
baina ya tabaka ya “Ectoderm” ya nje na tabaka ya
“Entoderm” ya ndani yenye tabaka mpya ambayo ni tabaka
ya kati ( Mesoderm ).
Kutokana na kudhihiri
kwa mchirizi wa kwanza, huanza kufanyika kwa chombo cha
mishipa ya fahamu na ncha ya uti wa mgongo. Pia
hufanyika tabaka ya kati ( Mesoderm ), na kijusi huanza
kufanyika viungo. Ama pasipokuwepo au kutofanyika kwa
mchirizi wa asili, basi viungo hivyo havifanyiki, na kwa
hiyo kisahani cha awali cha kijusi hakiwezi kugeuka
kuingia kwenye kipindi cha kufanyika kwa viungo ikiwemo
chombo cha mishipa ya fahamu.
Kutokana na umuhimu wa
mchirizi huu, tume ya Warnek ya Uingereza ( inayohusika
na uchevushaji wa binadamu na vijusi ), imeufanya kuwa
ni alama yenye kutenganisha baina ya wakati ambao
madaktari na watafiti wanaruhusiwa kufanya majaribio kwa
vijusi vya awali vinavyotokana na ongezeko la
uchevushaji usio wa asili katika bomba ( visahani ).
Wakati wa kudhihiri kwa mchirizi wa asili na kutokana na
nguvu zake kubwa hudhihiri yafuatayo :
Katika wakati ambao
kijibomba cha mishipa ya fahamu kinapojifunga,
hudhihiri “Otic Placode” na “Lens Placode”.
Ubongo hufanyika katika
theluthi mbili za juu ya kijibomba cha mishipa ya fahamu
wakati ambapo uboho hufanyika katika theluthi ya chini,
hiyo ni kwa ngazi ya ukubwa wa mwili ( nne – tano ).
Kwani ukubwa wa mwili (Somirtes) mine ya kwanza hufanya
sehemu ya tako la fuvu.
Hufanyika tabaka ya
Mesoderm ambayo huwa kwa wingi pembezoni mwa mhimili wa
kijusi chenye ukubwa wa mwili (Somites) ambayo hufanya
uti wa mgongo na tishu. Pia hutokeza mwanzo wa ncha za
juu na chini, nazo ndizo zenye kufanya chombo cha umbo
na tishu. Pia hufanyika chombo cha mkojo na uzazi. Pia
hufanyika kifuniko cha tumbo la ndani, kifuniko cha
mapafu mawili na kifuniko cha moyo kwa mpangilio.
Kadhalika hufanyika mishipa ya damu, moyo na tishu za
chombo cha usagaji chakula.
Kama hivi ikiwa mchirizi
wa asili ni alama muhimu ya kuanza kudhihiri kwa tishu
za kijusi na kufanyika kwa tabaka tofauti ikiwemo
viungo. Kwa kweli kile kinachojulikana kuwa ni kipindi
cha kufanyika kwa viungo ( Organogenesis ) hakianzi ila
baada ya kufanyika kwa mchirizi wa asili, (AL
MIIZAAB AL ASWABII) na
ukubwa wa mwili, na huendelea kuanzia wiki ya nne hadi
mwisho wa wiki ya nane, kwani kijusi katika kipindi
hicho kinakuwa kimekamilika kuwa na vyombo vyote muhimu,
na viungo vyake vinakuwa vimeshafanyika isipokuwa vitu
vidogo vidogo na ukuaji.
Mwisho wa mchirizi wa asili
(Primitive Streak):
Mchirizi wa asili
unapokaribia kumaliza kazi yake hiyo katika wiki ya nne
hadi uanze kutoweka na kubakia umejificha katika eneo la
kifupa ndugu
katika kijusi kisha katika
mtoto, na hutoweka isipokuwa athari ndogo ambayo haiwezi
kuonekana kwa macho ya kawaida.
|