|
|
|
UTOSI |
|
Mwenyezi Mungu Amesema : “Sivyo
hivyo! Kama haachi, Tutamkokota kwa nywele za utosi.
Utosi muongo, wenye madhambi.” ( Aya za 15-16
Suratul Alaq ). |
|
UKWELI WA KISAYANSI :
Ubongo wa binadamu una
vigawanyo vinne vikuu ambavyo ni : “Frontal Lobe”,
“Occipital Lobe”, “Temporal Lobe”, na “Parietal
Lobe”. Kila sehemu ina kazi yake peke yake
inayotofautiana na nyengine. Wakati huo huo, sehemu zote
hizo ni zenye kukamilishana. Sehemu ya mbele ndio yenye
kusifika na nyenzake katika wanyama, kwani ndio sehemu
zinazohusika na tabia, maneno yaliyoendelea na ndio
iliyowazi kwa upande wa uchunguzi na kikazi. Ni sehemu
yenye vituo kadhaa vya akili ambavyo vinatofautiana kwa
upande wa eneo na kazi. Na utandu wa mbele wa utosi (Pre-Frontal
Cortex), uko moja kwa moja nyuma ya paji la uso, nao
ndio sehemu kubwa ya sehemu ya mbele ya ubongo na kazi
yake inashikamana na kujenga haiba ya mtu . Pia ina
athari kubwa katika kuainisha hatua (Initiative)
na hukumu (Judgment). Kisha sehemu ya kuendeshea
maneno ya broka ( Motor Speech Area of Broca)
yenye kuratibu harakati baina ya viungo vinavyoshiriki
katika zoeza la usemaji mfano wa koo, ulimi na uso.
Kisha maeneo ya harakati
yanayokusanya sehemu ya
mbele ya jicho (Frontal Eye Field) ambayo hutoa
msukumo unaoambatana na macho kuelekea kwenye upande
unaokabiliana nao na sehemu ya kuendeshea viungo vikuu
na visaidizi (Primary & Secondary Motor Areas).
Sehemu zote hizo mbili ni zenye kuhusika na uendeshaji
wa matakwa ya viungo. Kama hivi imethibika kuwa mwanzo
wa sehemu ya mbele ya utosi
iliyoko katika kina cha
utosi, ndio yenye kuelekeza tabia na yenye kuainisha
haiba. Kujeruhiwa kwake, kunaweza kusababisha mporomoko
wa vigezo vya tabia, kiwango cha kumbukumbu na uwezo wa
kutatua matatizo ya akili. |
|
UPANDE WA MIUJIZA:
Tatizo halikupata
ufumbuzi au kudhihirika namna yake isipokuwa hivi
karibuni katika zama za sayansi . Quran Tukufu
imeikusudia sehemu ya utosi au sehemu ya mbele ya
kichwa bila ya sehemu nyengine yoyote ya viungo kuhusika
na uongo, na kosa na uhalifu wake wa maneno machafu,
nako ni kukikamata kitu na kukivuta kwa nguvu ikiwa ni
taswira ya kukihukumu kiungo kinachohusika na tabia
katika binadamu. Ukweli huu wa kuhusishwa sehemu ya
mbele pekee kabla ya ugunduzi wa kazi yake ya kuelekeza
tabia na kupambanua haiba ya mtu hakufasiriwi na sudfa
wakati wa kuachishwa ziwa la mama.
Kwa hekima ya sheria ya
Mwenyezi Mungu, umekuwepo utosi huu na pengine kuna
uhusiano baina ya utosi wenye kusujudu kwa woga na tabia
iliyonyooka (Bila shaka sala ni yenye kuzuia mambo
machafu na maovu. Na kwa yakini, kumbusho la Mwenyezi
Mungu ni jambo kubwa kabisa, na Mwenyezi Mungu Anayajua
mnayoyatenda.)
Undani wa utosi na kazi ya sehemu
ya mbele ya ubongo, ni durusu ya miujiza ya Suratul
alaq. |
|
 |
|
Tafsili:
Kiarabu
 |
|
Kiingereza
Kifaransa Kijerumani Kispani Kituruki
Kiurdu
Kifarsi Kihausa |
|
|