|
Mwenyezi Mungu Amesema, “ Hakika
wale waliozikataa Aya zetu, Tutawaingiza katika moto.
Kila ngozi zao zitakapowiva, Tutawabadilishia ngozi
nyengine badala ya zile; ili wawe wanaonja (uchungu wa)
adhabu (maisha). Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu
na Mwenye hekima.” Aya ya 56 ya Suratul Nisaa.
Pia Mwenyezi Mungu amesema, “ Na
wakanyweshwa maji yachemkayo yatakayokata chango zao.”
Aya ya 15 ya Suratut Muhammad. |
|
UKWELI WA KISAYANSI:
Kabla ya gunduzi za
kisayansi, kulikuwa na imani kuwa mwili wote ni wenye
kuhisi maumivu. Haikuwa wazi kwa yeyote kuwa kuna mwisho
wa nava katika ngozi ambazo zinahusika na uchukuzi wa
hisia na maumivu, hadi ulipogunduliwa mchango wa mwisho
wa nava katika ngozi, nacho ni kiungo muhimu mno kwani
kina idadi kubwa ya nava. Dk. Head ameigawa hisia ya
ngozi katika makundi mawili : Hisia nyeti (EPICRITIC)
inayohusika na kupambanua hisia ya
mguso mdogo na tofauti ndogo ya joto, na hisia kuu (PROTOPATHIC)
inayohusika na maumivu na kiwango kikubwa cha joto. Na
kila hisia kati ya hizo mbili, inafanya kazi kwa aina
tofauti ya sehemu za nava . Pia kuna seli maalumu
inayohusika na ugunduzi wa mabadiliko maalumu ya
mazingira (RECEPTORS). Nazo zimegawika katika
sehemu nne : Seli zinazoathirika na mazingira ya nje (EXTEROCEPTORS).
Hizi zinahusika na hisia ya kugusa na zinakusanya
vijisehemu (MEISSNERS CORPUSCLES) na vijisehemu (MERKELS
CORPUSCLES). Seli za nywele na mwisho wa (BULBES
ERAUSE END) inayohusika na baridi. Silinda ya
Ruffini, (RUFFINI’S CYLINDERS) inayohusika na
joto. Mwisho wa nava zenye kuchukua maumivu. Ngozi ni
sehemu tajiri mno kwa mwisho wa nava zenye kuchukua
maumivu na joto.
Pia wataalamu wa
uchunguzi wa mwili wamethibitisha kuwa mwenye kuungua
ngozi kikamilifu, basi hahisi maumivu makubwa kutokana
na kuharibika kwa mwisho wa nava wenye kuchukua maumivu,
kinyume na kuungua kidogo (kiwango cha pili), kwani
maumivu huwa makali zaidi kutokana na kuwa wazi kwa
mwisho wa nava. Pia wataalamu wa uchunguzi wa mwili
wamethibitisha kuwa michango midogo kwa ndani, haina
chenye kupokea hisia wakati ambapo zipo kwa wingi kwenye
eneo la kuta na eneo la nje la matumbo makubwa. Na
katika eneo hilo, kuna kiasi kikubwa cha vijisehemu
(vinavyofikia cubic cm 20400) ambavyo ni sawa na kiwango
cha ngozi ya nje ya mwili. Pia makutanio ya maumivu
(RECEPTORS) na sehemu nyengine za hisia zilizopo katika
michango ya tumbo, yanafanana na zile zilizopo katika
ngozi. |
|
UPANDE WA MIUJIZA:
(a)
Mwenyezi Mungu Amebainisha kuwa
ngozi ndipo mahali pa adhabu. Akaunganisha baina ya
ngozi na hisia katika aya ya kwanza na kwamba ngozi
inapowiva na kuungua na kupoteza mpangilio wake na kazi
yake, basi huondoka hisia ya maumivu ya adhabu. Basi
kubadilika kwa ngozi mpya iliyokamilika mpangilio wake
na iliyotimia kazi yake, mwisho wa nava – unaohusika na
hisia ya joto na maumivu ya moto – hutekeleza mchango
wake na kazi yake, ili kumfanya mtu huyu kafiri
anayezikataa aya za Mwenyezi Mungu Mtukufu aonje adhabu
ya kuungua kwa moto.
Sayansi mapya imegundua kuwa
mwisho wa nava unaohusika na hisia ya joto na maumivu ya
kuungua, hazipo kwa wingi isipokuwa kwenye ngozi. Na
hakuna hata mtu mmoja kabla ya kugunduliwa kwa darubini
na kuendelea kwa sayansi ya uchunguzi wa mwili, ambaye
angejua ukweli huu ulioashiriwa na Qurani Tukufu tokea
karne kumi na nne. Kama hivi unajitokeza wazi muujiza na
kudhihiri dalili za Mwenyezi Mungu .
(b)
Qurani Tukufu imewakamia
makafiri kwa adhabu ya maji yachemkayo yakatayo chango
zao katika aya ya pili. Imedhihirika siri ya makamio
hayo mwishoni kwa kugundua kuwa chango haziathiriki na
joto, lakini zikikatika, hutoka maji yanayochemka na
kuingia kwenye eneo lenye kiasi kikubwa cha mapokezi ya
joto na maumivu na kwenye mwisho wa nava na kufikisha
kwenye ubongo. Na wakati huo mtu huhisi kiwango cha juu
cha joto.
Kama hivi inadhirika wazi miujiza
ya kisayansi katika hisia ya maumivu kwa kukubaliana
baina ya ukweli wa tiba na miujiza ya Qurani Tukufu. |