Bodi ya Kimataifa Ya Miujiza Ya Kisayansi Ya Qurani Na sunna    
Risala yetu: Kudhihirisha miujiza ya kisayansi Na kuihakiki na kuichapisha.

Lugha

Ukurasa Kuu Muhtasari Wa Utafiti Kuhusu Bodi Wasiliana Nasi  

KUUMWA KWA KIWILIWILI

Mtume (S.A.W) amesema, “ Mfano wa Waumini katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao, na kuoneana imani kwao, ni sawa na kiwiliwili. Kikiumwa kiungo kimoja, basi mwili mzima hukesha na kupata homa.”

(Imepokelewa na Bukhari na Muslim na wengineo).

UHAKIKA WA KISAYANSI:

          Tafiti pevu na za kuendelea bila ya kusita za kisayansi, zimethibitisha ukweli wa kushangaza kuhusu maingiliano ya mwili wa binaadamu wakati wa kukabiliana na hatari kama vile kujeruhiwa au kuumwa. Imegunduliwa mistari ya kinga na kuitikia kikazi ambako kunatokea kwenye mwili wakati wa kiungo kati ya viungo vyake kuumwa au kujeruhiwa. Mshituko huo unakwenda sambamba na kiwango cha tabu ya kiungo kwa mwendo wa uwiano. Kwa kadri ya maumivu ya kiungo yanavyokuwa, ndivyo inavyokuwa nguvu ya mwili na kazi zake kwa ajili ya kuzuia kukomaa kwa maradhi na kufikia kupona kamili. Katika hali ya kujeruhiwa kwa kiungo, kwa mfano vituo vya ubongo huita (Tezi pituitari) ili itoe homoni inayotoa wito kwa (Tezi endokirini) ambazo hutoa mada za motisha na kuvitolea wito viungo vyote kutekeleza kazi zao kukiokoa kiungo chenye kuumwa. Mwili huelekeza  nguvu zake zote kukihudumia kiungo kinachouma. Moyo kwa mfano, huharakisha mapigo kwa uharaka wa mzunguko wa damu katika wakati ambao mishipa ya damu inajishika na sehemu za mwili zilizochoka na hupanuka mishipa ya damu iliyo jirani na kiungo kinachoumwa ili kukipatia mahitaji yake ya nishati, oksijeni, kiuavijasumu, homoni na baadhi ya asidi katika hali yake ya kuumwa kwa maana ya kubomoka na kuporomoka. Huanza kwa kubomoka kwa hazina ya mafuta ili chenyewe kiweze kukipa kiungo kinachoumwa mahitaji yake hadi kiweze kuyadhibiti maradhi na tishu ziweze kushikamana. Kisha baada ya hapo, mwili unarejea kujijenga wenyewe. Ishara zinazotoka kwenye jeraha ni sawa na malalamiko na kuomba msaada wa kweli zenye kupelekea kuchukuliwa. Huchipuka mapigo ya nava toka sehemu inayoumwa kuelekea kwenye ubongo ambako kuna vituo vya hisia, uthibiti unatokea wenyewe na kutoa mada za kemikali pamoja na tone la kwanza la damu lenye kumwaika mshipa wenye kukatika. Huitikia viungo vya mwili wote kila kimoja kwa mujibu wa kazi yake, na matokeo ni kuelekeza nishati ya mwili wa binadamu na kazi za viungo vyake kwa ajili ya kuhudumia kiungo hicho kinachoumwa.

UPANDE WA MIUJIZA:

          Mantiki  ya hadithi ndiyo yenye kutokea kitiba. Sehemu za mwili huitana zenyewe kwa zenyewe na kwa maana zote za kuitana. Mtume (S.A.W) anatoa habari kuhusu yanayopaswa kuwa na umma wa Kiislamu kuhusiana na kupendana, kuhurumiana na kuoneana imani kwa kutoa mfano wa mwili mmoja wakati kiungo kimoja kinapougua. Amebainisha kuwa vinaitana vyote kwa ajili ya kiungo hicho. Ametoa habari juu ya ukweli wa yanayotokea ndani ya mwili wa binadamu, kwani jicho lisingeweza kuuona kwa kutumia maneno yenye kuuelezea ukweli wa yanayotokea kwa maana zote zilizokuja katika lugha kwa mtindo wa kufanananisha ambao unaleta maana katika akili. Ni jambo la kushangaza kwa madaktari kutumia majina ya chombo cha nava ambacho kinachanganyika katika hali ya mwili kupatwa na hatari na maradhi na kuelezea ukweli wa kinachofanywa na mfumo huo na chombo hicho. Na tafsri yake ya neno ikawa ni: kupendana,  kuhurumiana na kuoneana imani, nayo ndiyo hayo hayo yaliyosemwa na Mtume (S.A.W) katika hadithi. Ametakasika Mwenyezi Mungu Aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na dini ya haki ili kuidhihirisha kwa dini zote na akampa aya za wazi na jumla ya maneno.

Seli zinaitikia wito wa sehemu inayoumwa nahushambulia gesi zinazoingia na kuziangamiza kasha kuzitoa .Miujiza ya kitiba katika Sunna tohara: mwili unatoa wito kwa kujeruhiwa na maradhi.

Tafsili: Kiarabu   

              Kiingereza   Kifaransa     Kijerumani      Kispani      Kituruki       Kiurdu    Kifarsi     Kihausa

Bodi ya Kimataifa Ya Miujiza Ya Kisayansi Ya Qurani Na sunna   (1428-2007)