|
|
|
KUUMBWA MTOTO KATIKA MAUMBO
TOFAUTI |
|
Mwenyezi Mungu Amesema :
“Mmekuwaje hamuweki Heshima ya Mwenyezi Mungu. Na hali
ya kuwa Amekuumbeni namna baada ya namna?”. (Aya
13-14 Suratul Nuh). |
|
UHAKIKA WA KISAYANSI :
Mtu wa kwanza kumsoma
mtoto wa kuku kwa kutumia lensi ndogo ni Harvey
katika mwaka 1651. Pia alidurusu vijusi vya mbawala.
Kutokana na ugumu wa kuainisha siku za kwanza za uja
uzito, akajua kuwa mtoto si chengine isipokuwa ni
takataka za mfuko wa uzazi. Katika mwaka 1672, Graaf
akagundua kokwa ndogo ndogo katika mayai ya uzazi ambazo
hadi leo zinaitwa kwa jina lake “Graafian Follicles”
na akakuta
vijiwe vidogo katika tumbo la
uzazi la sungura vyenye kufanana na kokwa ndogo ndogo.
Akajua kuwa mtoto sio takataka za tumbo la uzazi lakini
anatokana na mayai ya uzazi. Muundo huo wa ndani kabisa
alioujua Graaf si chengine isipokuwa ni vitundu
vidogo katika koja la seli za awali za mtoto (Blastocysts).
Katika mwaka 1675, Malpighi alikuta kijusi
katika yai la kuku akadhani
kuwa halihitaji vitu vya kurutubisha toka kwa jogoo.
Akadhania kuwa ni lenye kiumbe kidogo chenye kukua na
wala hakiumbiki katika maumbo tofauti. Kwa kutumia
darubini iliyoendelea zaidi, Hamm na
Leeuwenhoek, waligundua wadudu wa manii ya
binaadamu kwa mara ya kwanza katika historia mwaka
1677, lakini hawakuelewa ni ipi kazi yake hasa katika
uzazi. Pia walidhani kuwa yana binaadamu mdogo anayekua
katika tumbo la uzazi bila ya maumbo maalum ya uumbaji.
Katika mwaka 1759, Wolff alikisia kuwa ukuaji wa
mtoto unatokana na koja la awali la uumbaji lisilo na
umbo la kiumbe kilichokamilika. Katika mwaka 1775,
ulimalizika mjadala kuhusu dhana ya uumbaji uliokamilika
na ukafikiwa ukweli wa uumbaji katika maumbo. Majaribio
ya Spallanzani kwa mbwa, yakathibitisha umuhimu
wa wadudu wa manii katika zoezi la uumbaji. Kabla ya
hapo, ilitanda fikra ya kuwa wadudu wa manii ni viumbe
vya ajabu vinavyoishi kwa kutegemea viumbe vyengine, kwa
hiyo wamepewa jina la wanyama wa manii (Semen
Animals). Katika mwaka 1827, baada ya kupita miaka
150 ya ugunduzi wa wadudu wa manii, Von Baer
alikuta viyai vidogo katika vijiwe vya ovari ya mbwa
mmoja. Katika mwaka 1839, Schleiden na
Schwann walithibitisha kuwa uumbikaji wa mwili wa
binadamu unatokana na sehemu hai muhimu za uumbaji na
matokeo yake, na sehemu hizo zikaitwa Seli .
Baadae ikawa ni wepesi kufahamu ukweli wa uumbikaji wa
binadamu katika maumbo, kuanzia seli iliyorutubishwa
inayotokana na muungano wa manii na ovari. |
|
UPANDE WA MIUJIZA:
Aya tukufu inajuilisha
kuwa binadamu haumbwi ghafla kwa mujibu wa dhana
iliyokuwepo hadi karne kabla ya iliyopita, enzi za
Aresto kabla ya kuzaliwa kwa Kristo, bali anaumbwa
katika maumbo yenye makadirio thabiti yanayomkusanya
kila mtu licha ya kutofautina kwa makabila na kuambatana
kwa vizazi.
Historia ya sayansi ya
kijusi, inashuhudia kugongana kwa wataalamu katika
namna ya uumbaji wa binaadamu wakati ambapo Qurani
tukufu tokea karne ya kumi na saba, inatangaza kuwa
binadamu hawi ghafla, bali anakuwa kupitia maumbo
yaliyokisiwa kama ulivyo ujenzi wa jengo kwa mujibu wa
muundo uliowekwa. Sudfa haitafsiri maumbo yaliyokisiwa,
lakini inashuhudia hekima, kusudio na Uwezo wa Mwenyezi
Mungu na elimu yake ya vinavyomzunguka na uzuri wa
uumbaji Wake. Ama umoja wa maandalizi, mipango na
uthabiti wa maumbo, licha ya wingi wa makabila na
kuambatana kwa vizazi, basi tunahakikisha upweke wa
Muumba Mtukufu.
Fikra ya Aresto ya kuumbwa
kijusi
kutokana na damu ya hedhi,
iliendelea kuwepo hadi karne ya kumi na saba ambapo
aligundua darubini. Pamoja na hayo, wataalamu walidhani
kuumbwa kwake ni kamili bila ya maumbo tofauti. |
|
|
|
Tafsili:
Kiarabu
 |
|
Kiingereza
Kifaransa Kijerumani Kispani Kituruki
Kiurdu
Kifarsi Kihausa |
|
|