|
|
|
JUA KAMA NI
TAA NA MWEZI WENYE NURU |
|
Mwenyezi Mungu Amesema, “ Ni
mwenye kuleta baraka (kweli kweli) yule Aliyezijaalia
nyota mbinguni, na Akajaalia humo jua na mwezi
unaong’ara.” Aya ya 61 ya Suratul Furqan. |
|
UKWELI WA KISAYANSI:
Nishati ya jua (mtambo wa
nyuklia wa dunia). Hupatikana nishati ya jua kutokana na
kuungua kwa haidrojeni ambayo ndiyo sehemu yake kuu na
huigeuza kuwa helium ndani yake kwani wingi, shinikizo
na joto linalofikia digirii milioni 15, hayo yote
hupelekea kutokea kwa maingiliano ya nyuklia na
kuchanganyika kwa atom nne za haidrojeni kwa ajili ya
kutoa atom moja ya helium na inakuwa tofauti ya densiti
baina ya mada zenye kuingia katika maingiliano na
matokeo ya maingiliano huenea nishati ya sumaku umeme na
huenea juu ya jua mionzi yenye mawimbi madogo
yanayoambatana na mionzi ya kuonekana, mionzi myekundu
na mionzi ya zambarau. Hii ina maana ya kuwa jua
linategemea nishati yake toka ndani yake kupitia
kuchanganyika kwa kawaida kwa nyuklia katika hali kubwa
ya shinikizo, density na joto, kama kwamba ni mtambo
mkubwa wa nyuklia ili kuipatia ardhi mwangaza, ujoto na
nishati. Jua ni nyota, nayo ni kitu cha mbinguni
kinachong’ara na kutoa nishati chenyewe wakati ambapo
mwezi ni sayari, nayo ni kitu cha angani chenye mwangaza
thabiti kinachotoa mionzi inayoipokea toka kwenye nyota
na jua. Haya yanaambatana na matokeo ya kawaida ya
sayari. |
|
UPANDE WA MIUJIZA:
Maelezo ya Qurani tokea zaidi ya miaka elfu moja na mia
nne, yameashiria tofauti baina ya nyota na sayari, mfano
katika jua na mwezi. Nayo ndiyo yaliyofikiwa na
wataalamu wa falaki wa leo baada ya kugundua darubini na
kupiga picha za mwangaza kwa nyota na sayari katika
miaka michache iliyopita. Nyota si chengine isipokuwa ni
kitu cha mbinguni chenye kung’ara kinachotoa nishati
chenyewe wakati ambapo sayari ni kitu cha angani chenye
mwangaza thabiti na kinachotoa mionzi inayokipokea toka
kwenye nyota na jua. Na haya yanaambatana na matokea ya
kawaida ya sayari. Jua linahesabiwa kuwa ni mtambo
mkubwa wa nyuklia unaoelea angani kwa kasi kubwa wenye
mwangaza, nishati na joto yenye maumbo tofauti na yenye
kubadilika katika idadi na namna. Nalo sio kisahani
chenye kutoa mwangaza thabiti, bali ni taa yenye joto
kali. (Na Tukaifanya taa ing’arayo na yenye joto
kubwa). Suratul An Nabaa aya ya 13. Na mwezi ni
sayari yenye kuakisi mwangaza wa jua na hutoa nuru kwa
ardhi wakati wa usiku. Nalo ndilo ambalo limeelezewa na
Qurani tukufu katika aya mbili hizi. Basi ni nani
aliyemfahamisha Muhammad (S.A.W) ukweli huu? Hakika ni
Mwenyezi Mungu iliyotukuka shani Yake. |
|
|
|
Tafsili:
Kiarabu
 |
|
Kiingereza
Kifaransa Kijerumani Kispani Kituruki
Kiurdu
Kifarsi Kihausa |
|
|