|
Imehadithiwa na Imam Muslim
toka kwa Abdullah bin Furukh, amemsikia Aisha akisema
kuwa Mtume (S.A.W) amesema, “Kila mtu ameumbwa kutokana
na watoto wa Adam kwa viungo mia tatu na sitini.
Anayemkabiri Mwenyezi Mungu, akamhimidi Mwenyezi Mungu,
akasema La ilaha ila Allah, akamuomba maghfira Mwenyezi
Mungu, akaondosha jiwe kwenye njia ya watu au mwiba au
mfupa kwenye njia ya watu, na akaamrisha mema au
akakataza mabaya kwa viungo hivyo mia tatu na sitini,
basi anakwenda siku hiyo hali ya kuwa ameiokoa nafsi
yake na moto”.
Imepokelewa na Imam Ahmad kwa
kutegemea Abdulla bin Baraidah amesema: Nimemsikia Abi
Buraidah anasema: Nimemsikia Mtume (S.A.W) anasema “
Katika mwili wa binadamu, kuna viungo mia tatu na
sitini, ni juu yake kutoa sadaka kwa kila kiungo kati ya
hivyo. Wakasema: Ni nani anayeweza hayo, ewe Mtume wa
Mwenyezi Mungu? Akasema: Ni kohozi katika msikiti
analolifukia, au kitu anachokiondosha kwenye njia. Na
asipoweza kufanya hivyo, basi ni juu yake kusali rakaa
mbili za Adh dhuha, zitatosheleza.” |