|
UHAKIKA WA KISAYANSI:
Milima hapo awali
haikujulikana kwa lolote isipokuwa ni kama mkusanyiko wa
jiwe lilikwenda juu kwa usawa wa ardhi. Maana hiyo
iliendelea hadi Pier Bouger alipoashiria mwaka
1835 kuwa nguvu ya mvuto iliyosajiliwa kwa aina ya
milima ya Andes ni ndogo mno kuliko ilivyokuwa
ikitegemewa kutokana na ukubwa wa mkusanyiko wa jiwe
kama hilo. Akapendekeza udharura wa kuwepo kwa
mkusanyiko mkubwa zaidi wenye kuzama chini wa mada hiyo
hiyo ya milima ili iwezekane kutafsiri hali ya kipekee
katika uwezo wa mvuto. Katikati ya karne ya 19,
George Everest, aliashiria kuwepo kwa hali ya
kipekee katika matokeo ya kupima mvuto wa milima ya
Himalayas baina ya maeneo mawili tofauti. Everest
hakuweza kufasiri hali hiyo na akaipa jina la “Utata
wa India”. George Ebry akatangaza mwaka 1865
kuwa aina zote za milima katika ardhi ni mkusanyiko
wenye kuelea juu ya bahari kutokana na mada zilizoyeyuka
chini ya ardhi, na mada hizo zilizoyeyuka zinachukua
eneo kubwa zaidi ya mada ya milima. Kwa hiyo ni lazima
kwa milima kuzama kwenye mada hizo zilizoyeyuka zenye
eneo kubwa ili ziweze kulinda kusimama kwake.
Kama hivyo, elimu ya
jiolojia imegundua kidogo kidogo kuwa ardhi ni
mkusanyiko wa vipnde vilivyopakana vilivyoitwa mabamba
ya mabara. Pia imegundua kuwa milima mikubwa ni yenye
kuelea juu ya bahari kuliko milima yenye kunyumburuka
ambayo inachukua eneo kubwa zaidi huanguka. Pia
imegundua kuwa milima ina mizizi inayoisaidia kuelea na
kuyasimamisha mabamba hayo ili yasipinde na kutetereka.
Mwanajiolojia Van Anglin anasema katika kitabu
chake “Geomorphology” kilichochapishwa mwaka 1948
(uk.27) “ Inafahamika sasa kuwa ni lazima kuwepo kwa
mizizi katika (AL
SIYMAA) kwa mkabala wa
kila mlima uliopo juu ya ardhi”. Ama kwa upande wa kazi
au mchango wa milima katika kuituliza ardhi,
kumethibitishwa na msingi wa “ Uwiano wa Hydrostaty wa
ardhi”, kama ilivyoelezwa na mwanajiolojia wa Kimarekani
Dutton mwaka 1889 ambapo anasema kuwa miinuko ya
milima inazama ndani ya ardhi kwa kiasi ambacho
kinakwenda sambamba na muinuko na urefu wake. Uhakika wa
“mbao za ardhi” ulioungwa mkono mwaka 1969, umebainisha
kuwa milima inahifadhi uwiano wa kila bamba kati ya
mabamba ya ardhi. |
|
UPANDE WA MIUJIZA:
Katika wakati ambao
binadamu alikuwa hajui uhakika wa milima ambao
uliendelea hadi katikati ya karne ya kumi na tisa,
Qurani Tukufu imeweka wazi katika aya hii tukufu kuwa
milima inafanana na vigingi katika umbo na kazi. Hivi
karibuni umebainika ukweli wa kufanana huko kukubwa.
Kutokana
na kuwa milima ina sehemu
iliyodhahiri juu ya ardhi na sehemu nyengine iliyozama
ndani ya ardhi na kazi yake ni kuisimamisha sehemu
inayoelea. Kadhalika, milima ina sehemu iliyodhahiri juu
ya ardhi na sehemu nyengine iliyozama ndani yake
inayokwenda sambamba na muinuko na urefu wake. Na kazi
ya milima ni kuyasimamisha mabamba ya ardhi na kuyazuia
yasipinde na kutetereka kutokana na tabaka lililoyeyuka
chini yake. Kwa hiyo inadhihirika kuwa kitabu hicho ni
maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Muumba wa milima na
dunia kuthibitisha kauli yake Mwenyezi Mungu “ Oh!
Asijue Aliyeumba! Naye ndiye Avijuaye visivyojulikana na
vinavyojulikana.” Aya ya 14 ya Suratul Mulki. |