|
|
|
UHARAMU WA NYAMA YA NGURUWE NI
BAYANA YA KISAYANSI |
|
Mwenyezi Mungu Amesema :
“ Sema; “ Sioni katika yale niliyofunuliwa mimi kitu
kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni
mzoga au damu inayomwagika au nyama ya nguruwe, kwani
hiyo ni uchafu; au kile ambacho kwa kuhalifiwa amri ya
Mwenyezi Mungu kimechinjwa kwa jina la asiyekuwa
Mwenyezi Mungu. Lakini aliyelazimika kula pasipo
kupenda wala kuchupa mipaka, basi Mwenyezi Mungu ni
Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu.” Aya ya 145,
Suratul An-aam. |
UHAKIKA WA KISAYANSI
Imekuja elimu kudiriki
baadhi ya mambo yaliyokatazwa na sheria ya Kiislamu
iliyohifadhiwa na wafuasi wake karne kwa karne kabla ya
kugunduliwa kwa darubini na kwa mpangilio huo huo :
Mzoga ambao bakteria hukua ndani yake, damu ambayo
bakteria hukua ndani yake kwa kasi kubwa zaidi, hasa
ikiwa ni nyingi, na mwisho nguruwe ambapo katika mwili
wake hukusanyika jumla ya vijiumbe maradhi
visivyoondoka kwa kuoshwa. Mdomo ni maficho ya vijidudu,
bakteria na virusi vinavyokwenda kwa binadamu na
wanyama. Baadhi yake vinamhusu nguruwe, mfano wa kidudu
kiitwacho Trchinella, nywelenywele ziitwazo
Balantidium Dysentery, wadudu wa tumbo (Taenia
Solium) na mchango wa nguruwe (Spiralis).
Baadhi yake huingizwa kwenye maradhi mengi ya pamoja
baina ya binadamu ( Cysticercosis & Influenza) na
wanyama. Minyoo (Ascaris na Fasciolopsis
Buski) hupatikana kwa wingi nchini China. Maradhi ya
Balantidiasis hupatikana kwa wachunga nguruwe na
wenye kuchanganyika nao, na yanaweza kuenea kwa sura ya
mlipuko kama ilivyotokea katika moja ya visiwa vya
bahari ya Pacific baada ya kimbunga. Maradhi yanakuwepo
panapokuwepo nguruwe katika nchi zilizoendelea kiviwanda
kinyume na madai ya uwezekano wa kuushinda uchafu wake
kwa kutumia teknolojia mpya zinazoharamisha kula nyama
bila ya kibali, hasa nchini Ujerumani, Ufaransa,
Philippines na Venezuela. Kwa kula minofu ya nyama ya
nguruwe, (Trichinellosis) hupatwa na ugonjwa wa
Balantidium Dysentery. Kwani mke hubungua kuta za
matumbo kwa ajili ya kuweka mayai ambayo yanafikia kiasi
cha 10,000. Mayai hayo huingia kwenye misuli kupitia
damu na kugeuka kuwa ni vijiyai vyenye kuambukiza. Ama
kupata maradhi kupitia mchango wa nguruwe, ni kuwa hiyo
hupatikana baada ya kula minofu ya nguruwe mwenye
ugonjwa. Minyoo hukua kwenye mchango wa binadamu na
urefu wake unaweza kufikia meta saba, na unakuwa na
kichwa chenye miba inayosababisha kukwaruzika kwa kuta
za michango na mchupo mkubwa wa damu, na ana mirija
minne na shingo. Aina za mke huzaliwa kama kwamba ni
wanyama pekee na hufikia maelfu. Na katika kila mmoja
kati ya mnyama, huzaliwa zaidi ya mayai elfu moja iwapo
utakula Cysticercosis. Kupatwa na ugonjwa wa
minyoo ya tumbo la binadamu, hutokana na kula chakula
kilichoingia mayai na kutoa lava, na huingia katika damu
kupitia kiungo chochote. Na hatari yake hukisiwa kwa
mujibu wa umuhimu wake. Maradhi haya hayatokei kabisa
kutokana na kupatwa na mchango usio na miba katika
kichwa na wenye madhara madogo kabisa Taenia
Saginata ya ng’ombe. |
|
UPANDE WA MIUJIZA :
Nguruwe ni mwenye tabia
mbaya. Kuchukiwa na wasio na dini kumepelekea kumhesabu
kuwa ni muuaji wa alama za kheri. Visa vya kale
vimehadithia kuwa nguruwe alimuua Houras kwa Wamisri wa
kale na Adun kwa Wakanaan na Adonis kwa Wagiriki na Atis
katika Asia ndogo. Wafuga nguruwe katika Misri ya kale,
walihesabiwa kuwa ni watu walioijua vyema kazi yao.
Mchunga nguruwe haingii kwenye mfumo na
wala haoi isipokuwa
wanawake mfano wake. Na mwenye kumgusa nguruwe ni juu
yake kuoga. Nguruwe ni haramu kwa watu wa kitabu ingawa
wamekwenda kinyume. Lakini Qurani imetoa sababu ya
kukatazwa kula nyama yake kwa kauli yake Mwenyezi Mungu
“ Kwani hiyo (nyama) ni uchafu”. Neno uchafu ni
neno lenye kukusanya maana nyingi ikiwemo uchafu,
najisi, yenye maudhi, na yenye madhara. Ukatazo wa kula
nyama ya nguruwe japo kidogo kama ni chakula, umekuja
katika sehemu tatu nyengine. Kwanza kauli yake Mwenyezi
Mungu “Amekuharamishieni mzoga tu na damu na nyama
ya nguruwe na kilichotajiwa katika kuchinjwa kwake jina
la asiyekuwa Mwenyezi Mungu”. Lakini aliyefikwa na
dharura (ya kula vitu hivi) bila kutamani wala kupita
kiasi, basi yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni
Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu.” Suratul Al
Bakarah aya ya 173. Pili kauli yake Mwenyezi Mungu
katika aya ya 115 ya Suratul Nahl, “
Amekuharamishieni nyamafu tu (mzoga) na damu na nyama ya
nguruwe na (mnyama) achinjwae kwa jina lisilokuwa la
Mwenyezi Mungu. Lakini anayekosa budi
(anayeshurutishwa) bila kuasi wala kuruka mpaka, basi
(Mwenyezi Mungu atamsamehe); hakika Mwenyezi Mungu ni
Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu.” Tatu ni
kauli yake Mwenyezi Mungu katika aya ya 3 ya Suratul
Maidah, “ Mmeharamishiwa nyamafu na damu na nyama ya
nguruwe, na kinyama kilichochinjwa si kwa ajili ya
Mwenyezi Mungu, na kilichokufa kwa kusongeka koo, na
kilichokufa kwa kupigwa, na kilichokufa kwa kuanguka, na
kilichokufa kwa kupigwa pembe (na mwengine) na
alichokila mnyama (kikafa), ila mkiwahi kukichinja
(kabla hakijafa). Na (pia mmeharamishiwa) kilichochinjwa
panapofanyiwa ibada isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu (kama
mizimuni). Na ni (haramu kwenu) kutaka kujua siri kwa
kuagua kwa maboa (na yaliyo kama hayo). Hayo yote ni
maasiya.” Uharamu umekusanya vyote vinavyoliwa kama
mafuta. Kuharamishwa peke yake kwa Mayahudi
kunathibitisha kwamba asili ni kuingia kwake katika
nyama kama chakula. Mwenyezi Mungu Anasema, “Na kwa
wale walio Mayahudi, Tuliharamisha kila (mnyama) mwenye
kucha. Na katika ng’ombe na kondoo na mbuzi,
Tukawaharamishia shahamu (mafuta) yao isipokuwa ile
iliyobeba migongo yake (wanyama hao) au (iliyobeba)
matumbo au ile iliyogandamana na mifupa. Tuliwalipa
hivyo kwa sababu ya uasi wao. Na bila shaka sisi ndio
Wakweli.” Kuharamishwa kwa nyama kunaharamisha
mafuta hata kama ni chakula cha mnyama anayeliwa na
binadamu. Siku ilipoteremka Qurani, hakuna mtu aliyekuwa
akijua madhara ya nguruwe. Kwa hiyo inatoka wapi kinga
hiyo iliyokuja kwa sheria ikiwa haikuteremshwa kwa
ujuzi wa Mjuzi na Mwenye hekima! Mwenyezi Mungu Mweza
Anasema, “ Na watu wako wameikadhibisha chini Qurani
hali hiyo ni haki. Sema: “Mimi si mlinzi juu yenu”. Kila
khabari (iliyotajwa hapa) ina wakati wake (maalumu wa
kufika). Na hivi karibuni mtajua (haya).” |
|
 |
 |
|
|
Tafsili:
Kiarabu
 |
|
Kiingereza
Kifaransa Kijerumani Kispani Kituruki
Kiurdu
Kifarsi Kihausa |
|
|