|
UHAKIKA WA KISAYANSI:
1.
Wingu wa juu unayarejesha maji
yaliyogeuka kuwa mvuke katika hali ya mvua.
2.
Wingu wa juu unarejesha ardhini
vimondo vingi na kuvirejesha kwenye anga la nje.
3.
Wingu wa juu unairejesha mionzi
yenye kuua viumbe hai na kuisukuma mbali na ardhi.
4.
Wingu wa juu unaakisi mawimbi
mafupi na ya kati ya redio kuyarejesha ardhini. Kwa hiyo
tunaweza kuihesabu anga kama kioo chenye kuakisi miale
na sumaku umeme. Ni wenye kuakisi au kurejesha mawimbi
yasiyotumia waya na televisheni yanayorushwa angani na
ambayo hurejeshwa baada ya kurushwa angani baada ya
kuelekezwa kwenye tabaka za juu. Huu ndio msingi wa kazi
ya vyombo vya kurusha matangazo ya idhaa na televisheni
kupitia pande mbali mbali za ardhi.
5.
Wingu wa juu unafanana na kioo
chenye kuakisi joto. Unafanya kazi kama ni ngao ya
kujikinga na joto la jua wakati wa mchana. Pia unafanya
kazi kama ni pazia wakati wa usiku, huzuia joto la ardhi
lisisambaratike. Lau uwiano huu ukiteteruka, basi
itakuwa ni vigumu kuishi katika ardhi, ama kwa joto kali
mchana au baridi kali wakati wa usiku. |