Bodi ya Kimataifa Ya Miujiza Ya Kisayansi Ya Qurani Na sunna    
Risala yetu: Kudhihirisha miujiza ya kisayansi Na kuihakiki na kuichapisha.

Lugha

Ukurasa Kuu Muhtasari Wa Utafiti Kuhusu Bodi Wasiliana Nasi  

ARDHI YENYE MPASUKO

         Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “Na kwa ardhi inayopasuka (ikatoa mimea).”

       UKWELI WA KISAYANSI:

         Wataalamu wa jiolojia, wamegundua hivi karibuni kuwa ardhi  imegawika kwa wavu wa mipasuko ya kina katika vipande kumi na mbili vikuu vinavyopakana ambavyo kila kimoja huitwa bamba (plate) pamoja na mabamba mengine kadhaa madogo madogo yanayoitwa vijibamba (platelets). Mabamba hayo huelea juu ya tabaka ambalo ni kama limeyeyuka. Myeyuko (magma) huo hupanda baina ya  vina vya bahari na huongeza mada mpya kwenye mabamba mawili yaliyo jirani. Na kwa kuongezeka upande mmoja, hupungua upande mwengine daima kwa kuinamia chini ya upande wa bamba jirani. Kama hivyo, imebainika kuwepo kwa mipasuko mikubwa katikati ya bahari (Mid-Oceanic Rifts). Mipasuko hiyo huendelea hadi kuiziba ardhi yote, na kina chake kinaweza kufikia kilometa 150 kwa mujibu wa kina cha ardhi katika eneo lenye unene mkubwa zaidi. Pia imebainika kuwa mabara yote yanayojulikana leo pamoja na kuwa yana milima, huenda kwa mwendo wa mabamba yanayoyabeba kwa kukaribiana au kuwa mbali yenyewe kwa yenyewe, mwendo mdogo kabisa kufikia masafa yasiyopindukia idadi haba ya sentimeta kila mwaka lakini ni mwendo wenye kuendelea. Kwa mfano, mwanya wa Bahari ya Sham (Red Sea), unapanuka kwa sentimeta 3 kila mwaka na mwanya wa ghuba ya Califonia unaongezeka kwa sentimeta 6 kila mwaka. Kugongana kwa bamba la India na bamba la jirani yake baada ya kulika kwa bamba lililo baina yao, kumesababisha kufanyika kwa msururu wa milima ya Himalayas ambao una kilima kirefu zaidi duniani. Inaaminiwa hivi sasa kuwa  mabara mapya, yote yalikuwa ni kitu kimoja kilichoshikamana tokea miaka milioni 200 na kuwa ni bara moja pekee lililo kubwa na bahari moja yenye kulizunguka lote. Kwa kugawanyika kwake mpasuko wa asili ukapewa jina la mpasuko wa katikati ya Atlantic (Mid-Atlantic Ridge) na hadi leo ni eneo la harakati pevu za volkeno.

       UPANDE WA MIUJIZA :

            Mipasuko ya katikati ya bahari (Mid-Ocean Rifts),  haikugunduliwa isipokuwa baada ya vita vya pili vya dunia na imeelezewa kwenye nadharia ya “ Mabamba ya Tektonic” (Tectonic Plates)  iliyowekwa mwishoni mwa miaka ya sitini na mwanzoni mwa miaka ya sabini ya karne iliyopita tu. Kwa upande wa kisayansi, mipasuko hiyo inayoendelea kina chake chini ya kina cha ardhi, ni alama kubwa zaidi ya gamba la ardhi. Kwa hiyo Qurani Tukufu inahesabiwa kuwa ndio iliyotangulia kuashiria uhakika huu uliojificha chini ya ardhi, na kuwa ni dalili tosha kwamba ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mjuzi Mwenye hekima.

Tafsili: Kiarabu   

              Kiingereza   Kifaransa     Kijerumani      Kispani      Kituruki       Kiurdu    Kifarsi     Kihausa

Bodi ya Kimataifa Ya Miujiza Ya Kisayansi Ya Qurani Na sunna   (1428-2007)