|
UKWELI WA KISAYANSI:
Sayansi ya kileo chini ya mikono ya wataalamu wa viumbe
vidogo katika karne mbili zilizopita imegundua kuwa
kundi la bacteria, ukungu na virusi, havimfikii binadamu
isipokuwa kwa njia ya tendo la ngono la njia isiyo ya
kawaida. Ni kama kuwa na mahusiano mengi ya ngono yasiyo
maalumu baina ya wanaume na wanawake, na mahusiano ya
kimapenzi yasiyo ya kawaida baina ya wanaume kwa
wanaume, au baina ya wanawake kwa wanawake . Na iwapo
likitanuka duara la mahusiano hayo, basi jamii
inatishiwa na magonjwa ya kuambukiza yasiyopata kutokea.
Kwani vidudu hivyo vya maradhi hugeuka sifa zake bila ya
kusita jambo ambalo yanayfanya kuwa sugu kutibika. Pia
mwiliunashindwa kupambana navyo kwa sababu ya kutokuwepo
kinga ya mwili dhidi yake. Na pia yanaweza kutokea kwa
sura na sifa mpya katika mustakbali. |
|
UPANDE WA MIUJIZA:
Hadithi ya Mtume (S.A.W)
imetufichulia suna kuu ya kijamii inayoweza kutokea
katika jamii yoyote inayofanyika na utangulizi na
matokeo. Utangulizi: Kuenea mahusiano ya haramu kama
zinaa na mahusiano yasiyo ya kawaida katika jamii na
kutoyaharamisha na kuyaridhia, na kisha kuyatangazia.
Nalo ndilo lililopewa jina la kuhalalisha ngono, nayo
ndiyo yaliyomo kwenye kauli yake (S.A.W) “
Haukudhihiri uchafu katika kaumu katu hata
wakautangazia). Matokeo yanayotokana na zinaa hiyo,
ni kuenea kwa maradhi ya ngono na kutapakaa kwa sura ya
kuambukiza kwa hatari, na kudhihiri kwake katika sura
nyengine katika vizazi vinavyofuatia. Nayo ndiyo
yaliyomo kwenye kauli yake (S.A.W) : “Isipokuwa
itaenea tauni na maradhi kwao ambayo hayakuwahi kutokea
kwa waliowatangulia ambao wamepita”. Haya yametokea
katika miaka hii katika jamii nyingi za Magharibi.
Yameenea kwa mahusiano ya haramu na yasiyo ya kawaida,
na wao wakayaridhia kama ni tabia ya kijamii, bali
wameyatangazia kwa kila njia za matangazo zilizopo. Dk.
Shofield katika kitabu chake cha maradhi ya ngono
anasema: Umeenea urahisi wa jamii kuelekea kwenye
matendo yote ya ngono, na wala hakuna hisia yoyote ya
haya kutokana na zinaa na kulawiti, au uhusiano wowote
wa ngono usio wa kawaida au ulioharamishwa. Bali vyombo
vya uenezi vimejaalia kuwa ni kitu cha aibu kwa mvulana
na msichana kuwa ni mwenye kujikinga. Kujikinga kwa
upande wa mwanamme au mwanamke katika jamii za
magharibi, limekuwa ni jambo la kuonewa aibu na mtu.
Vyombo vya habari vinatoa wito na kuhimiza zinaa kwa
kuihesabu kuwa ni jambo la kimaumbile.
Idara ya maelezo ya
Uingereza inasema kuwa wenye mahusiano ya ngono yasiyo
ya kawaida, wametoka kwenye duara lao la siri na kuingia
kwenye duara la dhahiri, na wamekuwa na klabu zao, baa
zao, mabustani yao, fukwe zao, mabwawa yao ya kuogelea
na hata vyoo vyao.
Yameandikwa mamia ya
makala, vitabu, maigizo, hadithi na filamu zenye
kutukuza umalaya na mahusiano ya ngono yasiyo ya
kawaida, bali makanisa mengi ya Magharibi yameruhusu
zinaa na kulawiti, bali hufungwa ndoa baina ya mwanamme
na mwanamme mbele ya askofu katika baadhi ya makanisa ya
Nchi za Magharibi. Yameundwa maelfu ya jumuiya na vilabu
vinavyosimamia mambo ya wenye mahusiano ya ngono yasiyo
ya kawaida. Umefikiwa utangulizi wa tabia hii
inayoendelea. Je, yamefikiwa matokeo?
Naam, yamedhihiri kwao
maradhi ya zinaa katika sura ya maambukizo
yaliyowasababishia machungu mengi. Ulimwengu umeshuhudia
mawimbi makubwa ya kuenea kwa maradhi ya kaswende kwa
vipindi tofauti tokea kudhihiri kwa mara ya kwanza mwaka
1494, na kufyeka mamilioni ya watu katika karne ya 15
iliyopita na kuharibu maisha ya mamilioni ya watu
wengine. Bado vijidudu vya maradhi vinaendelea
kubadilisha sifa zake na vinamshambulia upya binadamu
katika ulimwengu wa leo. Kadhalika maradhi ya gono
yanaongoza maradhi ya kuambukiza, nayo ni kati ya
maradhi ya ngono yaliyoenea duniani na wenye kukata
uzazi kwa mwenye kushambulia, kwa hiyo unaitwa ugamba
mkubwa. Yote haya ni maradhi ya ngono yanayompata
binadamu anayekwenda kinyume na mafunzo ya mbinguni kwa
magonjwa na maradhi yenye kuuma. Kisha hivi mwishoni,
yamedhihiri maradhi ya ukimwi yanayotisha na yanayoua na
ambayo virusi vyake huangamiza chombo cha kinga katika
mwili wa binadamu. Kwa hiyo huangamiza viungo vyake
kimoja baada ya chengine katika msururu wa maumivu
ambayo hakuyajua binadamu hapo awali kabla ya
kugunduliwa kwa virusi mwaka 1983. Kama hivi yametokea
yaliyosemwa na Mtume (S.A.W). Hivyo hii sio dalili
nyengine ya kuwa Muhammad (S.A.W) ni Mtume wa Mwenyezi
Mungu kweli? |