|
|
|
HABA SODA NI DAWA YA KILA UGONJWA |
|
Toka kwa Mtume (S.A.W) amesema,
“ Hakuna ugonjwa wowote isipokuwa katika haba soda kuna
kupona kwake isipokuwa mauti.” |
|
UKWELI WA KISAYANSI:
Haba soda imetumika
katika nchi nyingi za mashariki ya kati na ya mbali
kama ni matibabu ya kienyeji tokea zaidi ya miaka
elfu mbili na ikawezekana kutolewa mkusanyiko wa dawa
uitwao Negelon kutokana na mafuta ya haba soda mwaka
1959 na Al Dakhani na wenzake. Mbegu ya haba
soda ina 40% ya mafuta thabiti katika uzito wake, 1.4%
mafuta mepesi na ina asidi kumi na tano, protini,
kalsiamu, chuma, sodiamu, na chokaa. Na kati ya madawa
yake yenye ufanisi ni : Themokenon, Dithemokenon,
Themohydrokenon na Themol. Mchango wa haba soda katika
kinga ya kimaumbile haukudhihirika hadi mwaka 1986
kupitia tafiti zilizofanywa na Dk. Al - Kadhi na
wenzake nchini Marekani. Kisha baaada ya hapo zikafuatia
tafiti katika nchi mbalimbali na katika nyanja nyingi
kuhusu mti huo. Al - Kadi amethibitisha kuwa haba soda
ina athari zenye kutoa nguvu kwa kazi za kinga. Kwani
kimezidi kiwango cha (Seli
za limfu) zenye kusaidia
na kuwa (Seli rejea
zenye kuzuia) kufikia 72%
kwa wastani. Pia imeboreka harakati ya seli za
kimaumbile zenye kuua kwa kiwango cha 74% kwa
wastani. Matokeo ya baadhi ya chunguzi mpya yamekuja
kuthibitisha matokeo ya tafiti za Al - Kadhi. Kati ya
hayo ni:
Yale yaliyochapishwa na jarida la
kinga ya dawa katika toleo la mwezi Agosti 1995 kuhusu
athari za haba soda kwa (Seli
za limfu za kibinadamu) nje
juu ya michupo kadhaa na juu ya harakati za kohozi
la
seli nyeupe za damu zenye viini vingi. Pia utafiti
uliochapishwa na jarida la kinga ya dawa katika toleo la
mwezi wa Septemba mwaka 2000 AD (10) kuhusu
athari za kinga za mafuta ya haba soda dhidi ya kupatwa
na virusi vyenye kukuza seli ( cytomegalovirus)
katika panya. Mafuta ya haba soda yalipofanyiwa
majaribio kama ni kiua virusi na hasa seli za kimaumbile
zenye kuua, seli kubwa za kohozi na zoezi la kufanyika
kohozi. Pia yaliyochapishwa na jarida la saratani la
Ulaya katika toleo la Oktoba mwaka 1999 kuhusu athari za
mkusanyiko wa Themokenon katika tumbo la panya. Pia
yaliyochapishwa na jarida la tafiti za dawa za saratani
katika toleo la Mei 1998 kutokana na mada za haba soda
kama ni dawa ya kumalizana na saratani. Kadhalika
yaliyochapishwa na jarida la Athno la madawa katika
toleo la Aprili 2000 kuhusu athari za sumu na kinga
kutokana na dawa ya Ethanol kutokana na mbegu za haba
soda. Pia yaliyochapishwa na jarida la mimea ya tiba
katika toleo la mwezi wa Februari mwaka 1995 kuhusu
athari za mafuta thabiti ya haba soda na mpangilio wa
Themokenon kwa vipira vyeupe vya damu, na tafiti
nyengine mbali mbali katika uwanja huo. |
|
UPANDE WA MIUJIZA:
Mtume (S.A.W) amesema
kuwa katika haba soda kuna matibabu ya kila ugonjwa.
Katika mtiririko wa hadithi zote, neno ugonjwa
halikuainishwa na limekuja katika mtiririko wa
kuthibitisha, kwa hiyo tunaweza kusema kuwa katika haba
soda kuna sehemu ya kupona kwa kila ugonjwa. Na
imethibiti kuwa chombo cha kinga mwilini ndio mpango
pekee wenye kumiliki silaha maalumu ya kumalizana na
kila ugonjwa, kwa kina mpango wa kinga ya kipekee au ya
kimaumbile yenye kumiliki ufanyaji wa viuavijasumu
maalumu kwa kila kiumbe chenye kusababisha maradhi na
kuunda silaha ya seli maalumu zenye kuua.
Imethibitika kupitia
tafiti za kivitendo kuwa haba soda huchangamsha kinga ya
kipekee. Kimepanda kiwango cha seli zenye kusaidia, na
seli zenye kuzuia, na seli za kimaumbile zenye kuua.
Nazo zote ni ( Seli
za limfu) zenye kuhusika
zaidi na zenye ufanisi, kwa kiasi cha 75% katika utafiti
wa Al-Kadhi. Tafiti zilizochapishwa katika machapisho ya
kisayansi zimethibitisha ukweli huu, kwani zimeboreka (
Seli za limfu )
zenye kusaidia na seli za
kohozi. Pia umezidi mkusanyiko wa Enterveron na
Enterloken 1,2 na kuboreka kinga ya seli. Ubora huo
umedhihirika katika chombo cha kinga kwa athari yenye
kuangamiza kwa dawa ya haba soda kwa seli za saratani na
baadhi ya virusi. Pia kuboreka athari za ugonjwa wa
michango ya Bilharzia. Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa
katika haba soda mna dawa ya kila ugonjwa, na
inatendeana na kila chenye kusababisha maradhi na
inamiliki utoaji wa kupona kamili au sehemu ya kila
maradhi.
Kama hivi umetukuka
ukweli wa kisayansi katika hadithi hizi tukufu ambazo
hakuna hata mtu mmoja aliyeweza kuzidiriki mbali ya
kuzisema tu na kuwazungumzia watu tokea karne kumi na
nne isipokuwa Mtume (S.A.W) aliyetumwa na Mwenyezi
Mungu. Amesema kweli Mwenyezi Mungu aliyesema, “ Na
wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake). Hayakuwa
(haya anayoyasema) ila ni wahyi (ufunuo) uliofunuliwa
(kwake).” Suratu Nnajmi aya za 3 – 4. |
|
|
|
Tafsili:
Kiarabu
 |
|
Kiingereza
Kifaransa Kijerumani Kispani Kituruki
Kiurdu
Kifarsi Kihausa |
|
|