|

Hotuba ya Mheshimiwa Dk./ Abdullah bin Abdel
Aziz Al-Muslih
Katibu Mkuu wa Bodi ya Kimataifa ya Miujiza ya
Kisayansi katika Qurani na Sunna.
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwenye kuneemesha
neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo.
Mabibi
na mabwana: Wageni wa eneo hili lenye baraka.
Wafuasi wa miujiza ya kisayansi katika Qurani na Sunna; ulimwenguni
kote. Nakuamkieni kwa maamkizi ya Kiislamu: Assalamu Aleykum wa Rahmatul
llahi wa barakatuh. Wabaadu…
Hii leo
wameitikia wito wenye shime na miujiza ya kisayansi katika Qurani na
Sunna duniani toka ulimwenguni kote na wamekutana pembezoni mwa Al
Kaabah na chini ya kivuli cha Msikiti Mtukufu wa Makka na wamekusanywa
na majengo ya Jumuiya ya dunia ulimwengu wa Kiislamu ili mkutano huu
utoe bodi ya kimataifa ya miujiza ya kisayansi katika Qurani na Sunna.
Hakika ni elimu. Je, hivyo elimu ni nini zaidi ya mwenye kujitolea
mhanga mwenyewe.
Hakika ni yakini. Je, kuna mwenye kuizuia yakini isipokuwa aliyeridhia
ujinga kuwa mwenzake.
Hakika ni muono wa mwenye kuangalia kwa makini dalili zilipokelewa
zilizo thabiti :
Dalili za kuona na dalili za kuandikwa.
Dalili katika ulimwengu, binadamu na maisha katika undani wenye
kushangaza na katika mpangilio wake katika ufalme huu, mwenye kutasabahi
kwa kumshukuru Mola wake.
Dalili katika kitabu hiki na sunna zimetuzungumzia kuhusu ukweli huu
katika maoano kamili na mshikamano mzuri pamoja na kuwa zimeteremka
katika wakati ambao haikuwa katika uwezo wa binadamu hata katika elimu
yao kuyajua wala kuujua na wala kuuzunguka ukweli huo.
Hakika ni hoja kubwa yenye kujulisha kuwa aliyeumba ulimwengu ndiye
ambaye ameishusha Qurani.
Hakika risala ya eneo hili la kimataifa ni kutubainishia ukweli huu
wenye kung’aa na kuwa ni kivukio cha kuifikia elimu ambayo kwayo
tutafikia kumhudumia binadamu katika kutafuta yanayowafaa watu waishi
katika ardhi, na tuuthibitishie ulimwengu kuwa dini yetu ni dini ya
elimu na maarifa. Inatafuta haki na inalingania kwenye ubunifu,
maendeleo na kuchukua sababu ya kuwa juu kimada na kutengeneza ustaarabu
kwa ajili ya maisha mazuri ya binadamu yenye uadilifu na elimu kuwa ni
kitumishi kwa watu yenye kuwasaidia, na sio tegemezi la kubomoa na
sababu ya kuangamiza. Kwa hiyo watu wote watakuwa katika usalama na
amani. (Hakika hii Qurani inaongoza kwa yale ambayo yamenyooka na
inawabashiria Waumini wanaofanya mema kuwa wana ujira mkubwa.)
Ama nyinyi wanazuoni, watafiti na watu wa kawaida wa eneo hili la
kimataifa!
Enyi wenye shime ya kushikana na eneo hili ambalo ni kwa ajili yenu na
lenu na kutoka kwenu na kwenda kwenu! Ni juu yenu kutoka kwangu na ndugu
zangu wanazuoni, watafiti na watu wa uongozi katika bodi ya dunia ya
miujiza ya kisayansi katika Qurani na Sunna. Tunashukuru fadhila, na kwa
nini isiwe hivyo? Kadhalika mkiwa mashahidi wa Mwenyezi Mungu kwa uungu
wake, majina yake, sifa zake na neema zake tukufu (Ameshuhudia
Mwenyezi Mungu kuwa hakuna Mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa
yeye Mwenyezi Mungu na malaika wake na wenye elimu mwenye kusimamia kwa
uadilifu hakuna Mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye mwenye
nguvu na mwenye hekima.)
Bodi hii ambayo ni jumuishi ianayokusanya vigogo wa wanazuoni
na wajuzi wa hali ya juu kati ya watafiti katika tafiti za miujiza ya
kisayansi katika Qurani na Sunna. Katika bodi hii, wanakutana vigogo wa
kisayansi wa kimataifa kwa suala hili muhimu kati ya masuala ya dini
yetu na sunna za Mtume wetu (S.A.W) kumuita kila mwenye uwezo wa kwenda
katika njia hii iliyo sawa na mavuno mazuri kwa ajili ya kuinua haki na
kudhihirisha ukweli na kugundua Aliyoyaweka Mwenyezi Mungu katika dunia,
na maisha na viumbe, jambo ambalo litafaidisha watu na kufichua neema za
Mwenyezi Mungu kwetu ambazo ameziweka katika ufalme wake. ( Yeye
ndiye Aliyekuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi ). ( Sema ewe
Muhammad! Angalieni vilivyomo mbinguni na ardhini ).
Bodi ya dunia ya miujiza ya kisayansi katika Qurani na Sunna
imejipa jukumu kwa mujibu wa njia ya kisayansi na misingi ya tafiti
katika miujiza ya kisayansi katika Qurani na Sunna ambayo tunaweza
kuyafupisha kama ifuatavyo:
1-
Kuachana na vitu visivyo na vielelezo na nadharia na kukiuka kipindi
hiki na kuingia kwenye kipindi cha uhakika wa kisayansi ambacho
hakikubali kupingwa wala kubadilishwa.
2.
Kuwepo kwa maana dhahiri juu ya uhakika katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu
au Sunna Sahihi za Mtume (S.A.W).
3.
Kuunganisha baina ya uhakika huo na maana ya kifungu kwa mtindo mwepesi
na rahisi.
4.
Maana hiyo iwe kwa mujibu wa ufahamu wa Waarabu ambao Qurani
imeteremshwa kwa lugha yao.
5.
Kutotafiti katika mambo ya ghaibu ambayo ni Mwenyezi Mungu Pekee ndiye
Anayejua elimu yake ambayo tumeyaamini na tumekubali muktadha wake.
6
Tafsiri ya Qurani iwe kwa Qurani, kisha sunna sahihi, kisha kutokana na
mambo sahihi yaliyopokelewa toka kwa waliotangulia katika umma huu,
kisha kwa maana ya Lugha ya Kiarabu ambayo kwayo imeteremka Qurani
Tukufu.
Tunapenda kubainisha hapa kuwa shubha ambazo zimezushwa kuhusu
tafsiri ya kisayansi – na kadhalika wasiwasi uliotokea katika uwanja wa
miujiza ya kisayansi katika Qurani na Sunna – ni uhakiki ambao kwa jumla
yake uko juu ya tafiti zisizo na mpangilio, kwani wenyewe wameingia
katika kuharakisha au kughafilika na baadhi ya misingi iliyowekwa, kwa
kujua kuwa tafiti kama hizo si chengine isipokuwa ni hali zisizo za
kawaida zenye kukataliwa. Kwa hiyo mazingira ya kimataifa ya miujiza ya
kisayansi katika Qurani na Sunna wakati unapoangaliwa utafiti kati ya
tafiti zinazowekwa kwenye sehemu yake kwa mujibu wa kukurubia kwake
kufikia shuruti za tafiti au kuwa kwake mbali na shuruti na misingi
hiyo.
Matatizo ya tafiti katika uwanja huu na uzito tunaoupata, tabu na
vikwazo vya uchapishaji, masuala yote hayo athari zake zinaondoka na
kupotea vumbi lake wakati tunapoona athari na matunda ya tafiti za
miujiza ya kisayansi katika Qurani na Sunna. Tunapaswa kutaja baadhi
yake kwa ajili ya kuwapa motisha watafiti ili wapite katika njia hii na
wainusuru dini ya Mwenyezi Mungu kwayo. Kati ya hayo ni:
1.
Athari kubwa yenye kuachwa katika nyoyo za
Waislamu, inayotafsiriwa kwa kuzidi yakini kwao wakati wanapouona
uhakika huo na wenye kushangaza, kwani umepokelewa juu ya ulimi wa Mtume
asiyejua kusoma wala kuandika Muhammad bin Abdullah (A.S). Kama hivi
tunazikuta kuwa ni kihimizo bora cha kushikamana na Qurani na Sunna na
kufuata muongozo wao.
2.
Ni jibu la kweli juu ya fikra zenye shaka juu ya
usahihi wa risala ya Muhammad, kwani kuuaridhi uhakika huo ulioelezwa na
Mtume asiyejua kusoma wala kuandika katika wakati ambao hauna maendeleo
ya kisayansi. Pia hakuna katika jamii wala mazingira aliyoishi athari
yoyote ya sayansi katika nyanja hizo za kidunia. Kwa hiyo miujiza hii ya
kisayansi ni uwanja wenye rutuba kwa ajili ya kuwakinaisha wataalamu
waadilifu kuwa Qurani Tukufu inatoka kwa Mwenyezi Mungu na ukweli wa
Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W).
3.
Ni jibu la kisayansi linaloambatana na dalili ya
wazi kuwa dini ya Kiislamu ni kweli dini ya elimu. Kwa himizo la Mtume
(SAW) - na uhimizo wake wa kuitafuta na kudokeza kwake juu ya fadhila
za wanazuoni – ametaja hakika nyingi za kisayansi na ameashiria siri
nyingi za kidunia juu ya maudhui ya fani nyingi katika upeo wa dunia na
hakuna hata mmoja hadi leo anayeweza kuthibitisha kinyume chake, yaani
maana za kidunia zilizokuja katika hadithi sahihi pamoja na ukweli wa
kisayansi uliofikiwa leo hii.
4.
Miujiza ya kisayansi ni sehemi nzuri kwa Waislamu
ili wafuatilizie utafiti, majaribio, kulinganisha na njia nyenginezo za
gunduzi za kisayansi na mipango ya kielimu. Wakati huohuo, hayo
yanapelekea kupanua duara la miujiza ya kisayansi katika Qurani na
Sunna.
5.
Pia miujiza hii ya kisayansi ni mkondo wa
kiusalama unaotoa matawi mengine ya ulinganio wa Mwenyezi Mungu katika
ulimwengu wa leo ambao ni ulimwengu wa elimu. Anayefuatilizia sababu za
watu wengi kuingia katika Uislamu, ambao walikuwa Wakristo au Mabudha au
Mayahudi, atakuta kuwa baadhi yao wameanza mwendo katika njia ya haki
kupitia kuangalia kundi la miujiza ya kisayansi katika Qurani na Sunna.
6.
Bila shaka hali ya kurejea kwenye dini ya Uislamu
kwa wale ambao wameghafilika, na kama hivi kusilimu kwa wasiokuwa
Waislamu, basi hayo yote yametokana na yakini ya Waislamu kwa dini yao
kurejea kwenye hali ya utukufu katika nafsi za vijana wa umma wa
Kiislamu baada ya mporomoko uliowapata baada ya kuanguka kwa ukhalifa wa
Kiislamu na kuwavaa wasiwasi wa ukoloni.
7.
Haya yote yanatukumbusha ukweli ambao hawendi
kinyume hata kidogo na yale aliyotufahamisha Mtume wa Mwenyezi Mungu
(S.A.W) kwa kauli yake: “ Kundi la umma wangu litaendelea kupigania haki
wakisaidiana hadi wa mwisho wao apigane na Masihu Dajalu, hawadhuru
mwenye kwenda kinyume nao au kutupa mkono hadi itakapokuja amri ya
Mwenyezi Mungu.”
Sisi, katika eneo hili la kimataifa, tunatangaza wito mkubwa wa
kweli wa kimataifa kwa wanazuoni, watafiti na wenye shime na uwanja wa
miujiza ya kisayansi katika Qurani na Sunna washiriki nasi kwa elimu
yao, rai zao na nasaha zao. Sisi pamoja na wao, ni washirika katika njia
hii. Na kwa ndugu zetu wanaoishi ugenini nje ya ulimwengu wa Kiislamu,
tunawapa wito maalumu wa kuwa wawe walinganiaji wa Mwenyezi Mungu katika
sehemu hizo kwa kutumia njia hizi za ulinganio zenye kuathiri kwa wenye
kufaidika kutoka sehemu hii kutokana na tafiti zilizofikiwa kwa kina.
Tunatumai kuwa tutafika pamoja na wote katika tovuti hili hadi iwe ni
dira ya tovuti katika uwanja huu na kiini chake.
Wito huu toka sehemu hii ya kimataifa wa kuijaalia anga ya
mitandao ya kimataifa ni sehemu ya kukaribisha inayowakusanyeni kwenye
meza ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume Wake (S.A.W).
Enyi ndugu! Kuweni askari wa Mwenyezi Mungu katika suala hili.
Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuwafikisha.
|