Bodi ya Kimataifa Ya Miujiza Ya Kisayansi Ya Qurani Na sunna    
Risala yetu: Kudhihirisha miujiza ya kisayansi Na kuihakiki na kuichapisha.

Lugha

Muhtasari Wa Utafiti Kuhusu Bodi Wasiliana Nasi  

 
   

       HOTUBA YA MHESHIMIWA KATIBU MKUU

 

Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema, “ Yussuf! Ewe mkweli ! Tueleze hakika ya ng’ombe saba wanene kuliwa na ng’ombe saba dhaifu. Na mashuke saba mabichi na mengine yamekauka, ili nirejee kwa watu wapate kujua. Akasema: “ Mtalima miaka saba mfululizo kwa juhudi (yaani limeni miaka saba kwa juhudi, kwani itaingia njaa kubwa baada ya miaka saba)

Mwenyezi Mungu Amesema : “Mmekuwaje hamuweki Heshima ya Mwenyezi Mungu. Na hali ya kuwa Amekuumbeni namna baada ya namna?”. (Aya 13-14 Suratul Nuh).

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “ Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu Anataka kumuongoza, Hufungulia kifua chake Uislamu; na yule ambaye Mwenyezi Mungu Anataka kumhukumu kupotea, Hufanya kifua chake kizito kinaona tabu kubwa (kufuata huo Uislamu); kama kwamba anapanda mbinguni (kusikokuwa na pumzi). Namna hivi Mwenyezi Mungu Anajaalia uchafu juu ya wale wasioamini. Aya ya 125 Suratul An-am

Mwenyezi Mungu Amesema, “ Hakika wale waliozikataa Aya zetu, Tutawaingiza katika moto. Kila ngozi zao zitakapowiva, Tutawabadilishia ngozi nyengine badala ya zile; ili wawe wanaonja (uchungu wa) adhabu (maisha). Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hekima.” Aya ya 56 ya Suratul Nisaa.

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “ Na milima kuwa kama vigingi (vya ardhi).”? Aya ya 7 ya Suratul Nabaa.

Mwenyezi Mungu Amesema : “ Sema; “ Sioni katika yale niliyofunuliwa mimi kitu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni mzoga au damu inayomwagika au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu; au kile ambacho kwa kuhalifiwa amri ya Mwenyezi Mungu kimechinjwa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliyelazimika kula pasipo kupenda wala kuchupa mipaka, basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu.” Aya ya 145, Suratul An-aam.

æóÇáúÈóÍúÑö ÇáúãóÓúÌõæÑö ﴿6﴾ ÓæÑÉ ÇáØæÑ

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: “ Naapa kwa mawingu yanayoleta mvua.” Aya ya 11 ya Suratul Tariq.

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “Na kwa ardhi inayopasuka (ikatoa mimea).”

Mtume (S.A.W) amesema : “ Haukudhihiri uchafu katika kaumu katu hata wakautangaza, isipokuwa itaenea baina yao tauni na maradhi ambayo hayakuwahi kutokea kwa waliotangulia ambao wamepita”

Toka kwa Mtume (S.A.W) amesema, “ Hakuna ugonjwa wowote isipokuwa katika haba soda kuna kupona kwake isipokuwa mauti.”

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “ Anazikutanisha bahari mbili (ya maji ya chumvi na ya maji matamu). Baina yao kuna kizuwizi, haziingiliani (zikaharibiana kabisa kabisa). Basi ipi katika neema za Mola wenu mnayoikanusha (kuwa si neema yake)? Katika hizo bahari mbili, hutoka lulu na marijani.”

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “ Naye (Mwenyezi Mungu) ndiye Anayeziunganisha bahari mbili; hii ni tamu, inayoondosha kiu, na hii ni yenye chumvi kali; na Akaweka kinga kati yao na kizuizi kizuiacho (zisiharibiane ila pale kiasi cha kukutana tu). Aya ya 53 ya Suratul Furqan.

Mwenyezi Mungu Amesema, “Au (amali zao zile mbaya) ni kama giza katika bahari yenye maji mengi, inayofunikwa na mawimbi juu ya mawimbi; na juu yake kuna mawingu; giza hili juu ya hili; anapoutoa mkono wake anakaribia asiuone (kwa kiza kilivyoshtadi) na ambaye Mwenyezi Mungu Hakumjaalia nuru, hawi na nuru.”

Mwenyezi Mungu Anasema, “ Basi Naapa kwa nyota zinazorejea nyuma. Zinazokwenda, kisha zikajificha.” Aya za 15 na 16 za Suratul At Takwy

Mwenyezi Mungu Amesema, “ Warumi wameshindwa. Katika nchi iliyo karibu (na nchi ya Bara Arabu. Nayo ni Shamu); nao baada ya kushindwa kwao watashinda. Katika miaka michache; amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla (yake) na baada (yake); na siku hiyo Waislamu watafurahi.”

Toka kwa Abu Hureira, Mtume (S.A.W) amesema, “ Kila binadamu ataliwa na udongo isipokuwa kifupa ndugu. Kwacho amezaliwa na ndani yake huumbwa.”

Mwenyezi Mungu Amesema : “Sivyo hivyo! Kama haachi, Tutamkokota kwa nywele za utosi. Utosi muongo, wenye madhambi.” ( Aya za 15-16 Suratul Alaq ).

Imehadithiwa na Imam Muslim toka kwa Abdullah bin Furukh, amemsikia Aisha akisema kuwa Mtume (S.A.W) amesema, “Kila mtu ameumbwa kutokana na watoto wa Adam kwa viungo mia tatu na sitini. Anayemkabiri Mwenyezi Mungu, akamhimidi Mwenyezi Mungu, akasema La ilaha ila Allah, akamuomba maghfira Mwenyezi Mungu, akaondosha jiwe kwenye njia ya watu au mwiba au mfupa kwenye njia ya watu, na akaamrisha mema au akakataza mabaya kwa viungo hivyo mia tatu na sitini, basi anakwenda siku hiyo hali ya kuwa ameiokoa nafsi yake na moto”.

Mtume (S.A.W) amesema, “ Mfano wa Waumini katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao, na kuoneana imani kwao, ni sawa na kiwiliwili. Kikiumwa kiungo kimoja, basi mwili mzima hukesha na kupata homa.” (Imepokelewa na Bukhari na Muslim na wengineo).

 

 

 

 

 

 

 

Bodi ya Kimataifa Ya Miujiza Ya Kisayansi Ya Qurani Na sunna   (1428-2007)