|
Muhtasari Wa Utafiti Wa Udaktari |
|
Maudhui |
Aya Na Hadithi |
Kuangalia |
|
SAYANSI YA UCHUNGUZI WA
MWILI INAAINISHA VITENGANISHI VYA MWILI |
Imehadithiwa na Imam Muslim
toka kwa Abdullah bin Furukh, amemsikia Aisha akisema
kuwa Mtume (S.A.W) amesema, “Kila mtu ameumbwa kutokana
na watoto wa Adam kwa viungo mia tatu na sitini.
Anayemkabiri Mwenyezi Mungu, akamhimidi Mwenyezi Mungu,
akasema La ilaha ila Allah, akamuomba maghfira Mwenyezi
Mungu, akaondosha jiwe kwenye njia ya watu au mwiba au
mfupa kwenye njia ya watu, na akaamrisha mema au
akakataza mabaya kwa viungo hivyo mia tatu na sitini,
basi anakwenda siku hiyo hali ya kuwa ameiokoa nafsi
yake na moto”. |
 |
|
UTOSI |
Mwenyezi Mungu Amesema : “Sivyo
hivyo! Kama haachi, Tutamkokota kwa nywele za utosi.
Utosi muongo, wenye madhambi.” ( Aya za 15-16
Suratul Alaq ). |
 |
|
KUUMWA KWA
KIWILIWILI |
Mtume (S.A.W) amesema, “ Mfano
wa Waumini katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao, na
kuoneana imani kwao, ni sawa na kiwiliwili. Kikiumwa
kiungo kimoja, basi mwili mzima hukesha na kupata homa.”
(Imepokelewa na Bukhari na Muslim
na wengineo). |
 |
|
HABA SODA NI DAWA YA KILA UGONJWA |
Toka kwa Mtume (S.A.W) amesema,
“ Hakuna ugonjwa wowote isipokuwa katika haba soda kuna
kupona kwake isipokuwa mauti.” |
 |
|
KIFUPA NDUGU
NA MCHIRIZI WA ASILI |
Toka kwa Abu Hureira, Mtume
(S.A.W) amesema, “ Kila binadamu ataliwa na udongo
isipokuwa kifupa ndugu. Kwacho amezaliwa na ndani yake
huumbwa.” |
 |
|
KUUMBWA MTOTO KATIKA MAUMBO
TOFAUTI |
Mwenyezi Mungu Amesema :
“Mmekuwaje hamuweki Heshima ya Mwenyezi Mungu. Na hali
ya kuwa Amekuumbeni namna baada ya namna?”. (Aya
13-14 Suratul Nuh). |
 |
|
HISIA ZA
MAUMIVU |
Mwenyezi Mungu Amesema, “ Hakika
wale waliozikataa Aya zetu, Tutawaingiza katika moto.
Kila ngozi zao zitakapowiva, Tutawabadilishia ngozi
nyengine badala ya zile; ili wawe wanaonja (uchungu wa)
adhabu (maisha). Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu
na Mwenye hekima.” Aya ya 56 ya Suratul Nisaa. |
 |
|
|
|
|
| |
|
|
| |
|
|
| |
|
|
| |
|
|